Carol Sonnie, mpenzi wa zamani wa mchekeshaji Mulamwah amesimulia jinsi mpenzi wake wa zamani alivyomtema hata baada ya kuonyesha upendo kwa mama mkwe.
Alizungumza hayo katika video kwenye mtandao wa You Tube, akiwa na marafiki zake watatu, mtayarishaji wa maudhui Mylee Staicey, Dorea Chege na Mwigizaji Morin, video iliyopewa jina "Craziest things we have done for love."
Wanne hao walifunguka kuhusu mahusiano yao ya zamani ambayo hayakufanikiwa, ingawa hawakutaja majina ya wapenzi wao.
Sonnie alisimulia jinsi alivyoshona nguo inayolingana na ya mama mkwe wake, lakini mpenzi wake wa zamani alimwacha baadaye. Alisema alifanya hivyo ili kuthibitisha mapenzi ya kweli kwa mpenzi wake.
“Ushawahi shona kitenge inafanana na mama mkwe? Unashona yako halafu unachukua vipimo vyake unapeleka kitenge ashonewe? ' Sonnie alisema.
Mama huyo wa mtoto mmoja alisema hadi alienda kanisani na mama mkwe wa zamani akiwa amevalia mavazi yanayolingana ila mambo yaliambulia patupu.
"Nakaanga chini najiuliza nini ilikuwa imeniingia kwa sababu ningechoose mamangu, the guy or my dad, but I just wanted to please the guy, alikuwa ni mama's boy. Na bado nikawachwa.'
Sonie aliongezea kuwa alikuwa anampenda sana mpenzi wake wa zamani, ingawa hakufichua utambulisho wake, na kuwaacha mashabiki wakidhania kuwa alikuwa akimzungumzia Mulamwah.