Mtayarishaji wa maudhui nchini Kenya Brenda Jons amerejea tena katika mitandao ya kijamii akitaja upya wa kiroho kuwa sababu iliyomfanya kuchukua mapumziko katika mitandao ya kijamii.
Katika chapisho la hivi majuzi kwenye mitandao ya kijamii, mtayarishaji wa maudhui alifichua kwamba alikuwa amechukua mapumziko ya miezi mitatu ili kuimarisha uhusiano wake na imani yake.
"Nilichukua miezi 3 ya mapumziko katika mitandao ya kijamii ili kuzama na kumsikia Mungu kwa ufasaha zaidi. Imekuwa likizo nzuri zaidi kuwahi kutokea." Brenda Jons alisema.
Jons alikiri kwamba kwa kipindi kikubwa, alikuwa ameruhusu mitandao ya kijamii kufafanua utambulisho wake, lakini aliona ni wakati wa kujitambua upya na imani yake akinukuu mstari kutoka kwa Biblia.
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, kabla hujazaliwa nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa,” akasema.
"Nilihitaji kujua mtu huyo ni nani. Ananifafanuaje na ni Mungu gani mwaminifu."
Wakati wa mapumziko, Brenda Jons alishiriki kwamba alijitolea kusoma Biblia kwa bidii zaidi, akiruhusu mafundisho ya Biblia kumuongoza.
Aliangazia umuhimu wa kutafakari na akataja mstari wa Injili kulingana na Yohana.
"Kondoo huitambua sauti ya mchungaji, yeye anayewalisha, kuwaongoza, na kuwalinda Sasa ninaweza kumsikia zaidi. Jinsi nzuri," alisema.
"Nimewakumbuka marafiki, Bwana amekuwa akikufundisha nini?" Aliuliza.