Raymond Omosa almaarufu kama Kenyan Prince amefunguka kuhusu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Princes Kerubo.
Kwenye mahojiano na Mungai Eve,katika chaneli yake 'Mungai Eve Media', mwanatiktoka huyo mbali na kuzungumzia safari yake ya utotoni hadi jinsi alivyoishia mitaani;Alifunguka kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake wa zamani Princess Kerubo ambaye anadai alimpenda sana lakini bado akamdanganya kwenye uhusiano wao.
Kulingana na Kenyan Prince,kudanganya kwenye mahusiano ya kimapenzi ni jambo la kawaida kati ya wanandoa na waseja. Kwake, hili si jambo kubwa kwani hutokea iwe kwa kujua au kutojua.
Alipoulizwa ikiwa anajuta kuumiza hisia za Princes Kerubo,Prince alishikilia msimamo wake na kudai kuwa hajutii lolote na matendo yake,bila huruma akidai hakuwahi kukosea hasa kwa vile walikuwa wamekaa pamoja kwa miaka 3.
Aidha mwanatiktoka huyo aliendelea kwa kusema kuwa alivumilia kwa muda wa miaka mitatu licha ya kuwa mwanadada huyo hakuwa anamridhisha kitandani.Hii ilimfanya kumcheza na hatimaye wawili hao kuachana.
"Nilikuwa kwenye uhusiano kwa miaka mitatu….nikifurahia ngono ya kusikitisha ili kuafikiana na mtu eti sababu mapenzi..." Kenyan Prince alimwambia Mungai Eve.
Mungai Eve alipomuuliza ni kwa nini anamchafulia Princes Kerubo jina,kijana huyo alieleza kuwa Princes Kerubo ndiye aliyeanzisha mtindo mzima na alikuwa akirudisha fadhila tu.
Raymond,ni miongoni mwa wafanyi biashara wa forex huku akitrendi kwenye mtandao wa tiktok,kutokana na hulka yake ya kuwaonyesha watu pesa kupitia video zake.