Mwanamume mmoja amechukua kwenye mtandao wa TikTok kueleza mbinu anazozitumia kuchukua pesa za nyanya yake kwa njia za udanganyifu.
Kwa mujibu wa mtumizi huyo wa TikTok, kila mara anapokosa pesa za matumizi yake, anatumia mbinu ya kuzima sauti katika simu ya nyanya yake na kumwambia kwamba ili kuirejesha sauti, anahitaji kulipia huduma hiyo na nyanya bila kujua kuwa anatapeliwa, anampa pesa ili aende akamnunulie sauti nyingine tena.
Kijana huyo alidai kwamba alimwomba nyanyake amtumie pesa ili anunue “tone ya mlio” wa simu yake.
Kijana anayepitia mpini @adamofori Tiktok alidai kuwa aliweka simu ya nyanyake kimya kwa makusudi.
Aliizima na kujifanya kwa bibi yake kwamba alihitaji pesa kununua sauti mpya za simu, kwa hivyo akampa pesa taslimu.
Kwa maneno yake;
"Niliweka simu ya bibi yangu kwenye kimya na kumwambia kuwa sauti ya simu yake ilikuwa imekamilika. Anapaswa kunipa pesa ninunue nyingine.”
Kutokana na ungamo lake, baadhi ya watumizi wa mtandao huo pia walieleza jinsi walikuwa wanatumia mbinu za udanganyifu kupata sifa kutoka kwa wazee wao.
Mmoja alieleza jinsi alifanya ukarabati wa kutoa flight mode kwa simu ya nyanyake, na bibi akaenda kutangaza kwa kijiji kizima jinsi mwanawe ni mtaalamu wa masuala ya simu.
Haya hapa baadhi ya maoni ya watu;
“Wakati fulani nilitoa simu ya bibi yangu kwenye flight mode, aliwaambia kila mtu jirani kuwa naweza kutengeneza simu.” Queenmother.
“Babu alienda ofisini kwa MTN na simu yake ndogo ili kubadilisha sauti yake ya mlio 😂😂Nilishtuka aliporudi kuniambia hivi.” Mwingine alisema.
“Swali langu ni je, ni wapi huwa hawa wazee wanatoa pesa zao, wengi wao wana pesa kutuliko sisi vijana” mwingine alilalama.