Mwanamuziki Stivo Simpleboy akieleza changamoto alizokumbana nazo katika safari ya mziki akibainisha kuwa haijakuwa safari rahisi kufikia mahali alipo kwa saa hii.
Alieleza mambo ambayo huwa yanamkasirisha na kumkatisha tamaa kama msanii ni watu kusema kuwa yeye sio msanii na kwamba hawezi na pia alisema badala ya kumkashifu mtu kama kuna uwezo wa kumsaidia anaweza.
“Kile huwa kinanikasirisha ni mtu kusema mimi siwezi, mimi ni kichaa,sina akili ilhali mimi naweza usichukulie mtu kwamba awezi. Kama unaweza kusaidia nisaidie badala ya kunikashifu,” alisema
Msanii huyo alibainisha kuwa kuna wakati alikuwa akiimba barabarani na kupata hela kidogo kidogo kutoka kwa wapita njia.
Simpleboy aliongezea kuwa watu wasingoje mtu kupoteza uhai wake hili waanze kuchanga pesa na wakati alikuwa hai na alitaka usaidizi akuna jambo walifanya hili kumsaidia.
“Kile naomba wakenya wanisaidie wasinichukulie mimi siwezi wakenya wanisaidie kama niko hai wasingoje niende chogomeo ndio sasa unapata mtu amechanga ndio stivo apumzike vizuri hapana, kama uko na uwezo mnisaide kama niko uhai usinisubiri nife.”
Stivo alisema kuwa wakenya awajui asili yake wanamjua yeye kama msanii na awajui mambo ambayo anapitia bila wao kujua na hivyo kuwaomba wakenya kumsaidia kimapato na kimziki pia.
Stevo simpleboy alisema kuwa ni matamanio yake kufanya kazi na msaa tajika hapa nchini Khaligraph Jones.