logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tuko hai! Zabron singers wazima madai ya kuhusika katika ajali

Japhet alisema ni mwezi mmoja sasa tangu waanze kusikia watu wakizungumzia ajali hiyo feki.

image
na Radio Jambo

Burudani31 May 2024 - 15:05

Muhtasari


  • "Watu wanatuua tukiwa hai. Nilikutana na watu kijijini kwetu wakisema walidhani tayari tumeaga dunia," alisema.

Waimbaji wa kikundi cha  Zabron singers, kupitia mwimbaji wao mkuu Japhet Zabron wamezima uvumi kuwa walihusika katika ajali ya barabarani.

Akizungumza na Wasafi TV, Japhet alifunguka;

"Watu wanatuua tukiwa hai. Nilikutana na watu kijijini kwetu wakisema walidhani tayari tumeaga dunia," alisema.

Aliendelea "Pia kumekuwa na habari kwenye mitandao ya kijamii kwamba tulipata ajali. Tulipata maswali mengi kutoka kwa mashabiki wetu wakituuliza nini kinaendelea."

"Nataka kuwaambia mashabiki wetu kwamba tuko hai, hakuna hata mmoja kati ya wanachama wetu aliyepata ajali. Tunamshukuru Mungu."

Japhet alisema ni mwezi mmoja sasa tangu waanze kusikia watu wakizungumzia ajali hiyo feki.

Waimbaji wa Zabron waliibuka kidedea kupitia wimbo wao wa 'Mkono Wa Bwana.' Tangu wakati huo, wamewafurahisha mashabiki kwa nyimbo nyingine nyingi miongoni mwao 'Uko Single' 'Sweetie Sweetie' 'Sisi Ndio Wale' miongoni mwa zingine.

Wanakikundi wengine ni pamoja na Victoria Zabron, Jamila Dotto, Samuel Joseph, Semroza Godfrey, Mark Bukuru, Grace Madata na Joyce Zabron.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved