Mwigizaji maarufu Jacky Vike aka Awinja Nyamwalo anasherehekea mwanawe anapofikisha umri wa miaka 7.
Mcheshi huyo wa mitandaoni, ambaye aliigiza jukumu la mlinzi wa nyumba katika kipindi cha Televisheni cha Papa Shirandula chenye mafanikio makubwa, hakuweza kuwa mtulivu katika siku kuu ya mwanawe.
Aliingia kwenye mitandao ya kijamii kushiriki mabadiliko ambayo mtoto huyo aliyemtaja kwa jina la Mosi, amepitia kwa miaka mingi.
“Suuuuuuuu!!! Siwezi Kuiweka Tulia ni Siku ya Kuzaliwa ya 7 ya mwanangu! Siwezi amini tumetoka Era ya Kupenda Spider man, he is now more into football! Ni yote anayofikiria,” Jacky Vike alishiriki.
Alifichua kuwa mwanawe alikuwa akipenda video za Spider man na kumlazimisha kununua vitu vya kucheza vilivyo na alama ya buibui.
Hii imebadilika sasa; mvulana huyo sasa ameingia kwenye soka, Ronaldo akiwa mchezaji wake kipenzi.
“Anampenda sana Christiano Ronaldo! Ni ndoto yake kukutana naye, Namba saba Mgongoni na Namba saba kwa miaka, sema sabasaba,” alifichua.
Mama mwenye furaha aliwaomba wafuasi wake wajiunge naye kusherehekea siku kuu ya mwanawe. Aliapa kusoma matakwa na maoni yote kwa Mosi, mtoto wake.
“Nyinyi nyote mnisaidie kumtakia Mosi siku njema ya kuzaliwa 7! Naahidi nitamsomea zote!”
Mcheshi huyo alisimulia maisha yake ya zamani alipokuwa akihangaika kumnunulia mwanawe vitu tofauti ambavyo vina picha za SpiderMan. Kuanzia vitu vya kuchezea hadi nguo zikiwemo soksi, vazi la usiku n.k.
“Niki imagine vile nilikua nang’ang’ana kutafuta vitu vya SpiderMan, si socks, si vikombe si nguo za kulala etc, nikiingia soko sehemu ya watoto kitu cha kwanza nauliza ni “Ukona anything ya spidermn?” sasa tuko hapa hataki hata kuziangalia,” alieleza.
Walakini, Jacky Vike anafurahi kwa mtoto wake, na hajutii kuwa katika safari hii ya maisha ya mtoto wake.
"Lakini ni safari ninayojivunia kuwa sehemu yake," mama alimalizia.