logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zawadi maalum, ujumbe mzuri kutoka kwa Michael Olunga zamsisimua mtangazaji Gidi

Gidi alijawa na bashasha baada ya kupokea zawadi maalum kutoka kwa nahodha wa timu ya Harambee Stars, Michael Olunga.

image
na Radio Jambo

Habari03 June 2024 - 05:34

Muhtasari


•Gidi alijawa na bashasha baada ya kupokea zawadi maalum kutoka kwa nahodha wa timu ya Harambee Stars, Michael Olunga.

•Gidi aliambatanisha ujumbe huo na picha na video za kifurushi cha zawadi alichopokea kutoka kwa Olunga.

alijawa bashasha baada ya kutumiwa zawadi maalum na Michael Olunga.

Mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, Gidi Ogidi alijawa na bashasha baada ya kupokea zawadi maalum kutoka kwa nahodha wa timu ya taifa ya Kenya ,Harambee Stars, Michael Olunga.

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 30 alimtumia Gidi jezi rasmi ya klabu ya Saudi-Arabia ambayo anaichezea, Al-Duhail ikiwa na maandishi ya jina lake ‘Olunga 14’ kwenye upande wa nyuma.

Wakati akitoa shukran zake kwa zawadi hiyo wikendi, Gidi alimshukuru nahodha wa Harambee Stars na kuitaja zawadi hiyo kuwa nzuri.

"Ni surpise iliyoje, zawadi kutoka Olunga, asante sana nahodha Michael Olunga kwa jezi nzuri," Gidi aliandika kwenye mtandao wa Facebook.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha na video za kifurushi cha zawadi alichopokea kutoka kwa Olunga.

Pamoja na jezi, mchezaji huyo wa Al-Duhail pia aliambatanisha barua nzuri ya maandishi kwa mtangazaji huyo wa kipindi cha asubuhi.

Katika ujumbe wake kwa Gidi, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alimshukuru sapoti yake na kukiri jinsi anavyomtambua.

"Gidi Gidi kama sisi sote tunavyokufahamu kutoka kwa unbwogable na Atoti. Asante kwa sapoti. Nakushukuru,” Olunga alisema kwenye barua aliyotia saini.

Kando na Gidi, nahodha huyo wa Harambee stars pia alituma jezi kwa Wakenya wengine maarufu na kuelezea shukrani zake kwao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved