logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Abel mutua asimulia alivyombusu Sarah Hassan

Sehemu ya pili ya mwisho wa kipindi changu  nilimpiga mate mbaya kwa class

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 June 2024 - 10:03

Muhtasari


  • •Mwigizaji wa Kenya Sarah Hassan, ambaye aliwahi kuigiza pamoja na Abel Mutua enzi hizo katika kipindi cha 'Tahidi High' kilichokuwa kikionyeshwa kwenye runinga ya Citizen kama 'Tanya', alitajwa kuwa mwigizaji mpole sana.
  • •Sehemu ya pili ya mwisho wa kipindi changu katika kipindi nilimpiga mate mbaya kwa class.

Mwigizaji  kutoka Kenya Abel Mutua, maarufu kwa mashabiki wake kama ‘Mkurugenzi’, alisimulia jinsi alivyoishia kumbusu mwigizaji Sarah Hassan.

Akizungumza katika mahojiano na Mic Check Podcast, Abel Mutua alikiri kumbusu mwigizaji huyo wa Kenya wakati wa  wakiigiza.

“Tanya  yaani Saraha Hassan alikuwa mpolite lakini Mungu ni nani kipindi chetu cha mwisho kabisa nikasema walahi huyu dem huyu vile amekua akininyima.

Sehemu ya pili ya mwisho wa kipindi changu  nilimpiga mate mbaya kwa class.” Abel Mutua alifichua.

Mwigizaji wa Kenya Sarah Hassan, ambaye aliwahi kuigiza pamoja na Abel Mutua enzi hizo katika kipindi cha 'Tahidi High' kilichokuwa kikionyeshwa kwenye runinga ya Citizen kama 'Tanya', alitajwa kuwa mwigizaji mpole sana.

Abel alikuwa sehemu ya uandishi wa kipindi hicho, alihakikisha kwamba alikuwa na njia yake na mwigizaji huyo, akikiri kwamba ni wakati ambao alifurahia kikamilifu.

Abel alisema kuwa ni katika onyesho yao ambapo kulikuwa na sehemu ya kipindi ilikuwa lazima tukio hilo lifanyike.

“Mungu ni nani. Sasa unakataa na script ndio imesema” Abel Mutua alifichua wazi, akionyesha furaha yake.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved