"Mpaka tukutane tena.." Mtangazaji Mbusii amuomboleza mpenzi wa reggea mwenzake, Jahmby Koikai

Njambi ambaye alikuwa mpenzi mkubwa sana wa muziki wa reggea alipoteza maisha usiku wa Jumatatu.

Muhtasari

•Huku akimuomboleza marehemu Jahmby, Mbusii alimtaja kama rafiki yake na kuitaka roho yake ipumzike kwa amani.

•Mbunge Jalang’o ametambua vita vikali vya Njambi na ugonjwa huo na kutaka roho yake ipumzike kwa amani.

Image: HISANI

Mtangazaji wa kipindi cha Mbusii na Lion Teketeke kwenye Radio Jambo, Mbusii ameungana na maelfu ya Wakenya kumuomboleza marehemu mtangazaji wa muziki wa reggea, Mary Njambi Koikai almaarufu Fyah Mummah Njambi.

Njambi ambaye alikuwa mpenzi mkubwa sana wa muziki wa reggea alipoteza maisha usiku wa Jumatatu, Juni 3 baada ya kuugua ugonjwa wa endometriosis kwa muda mrefu. Alikuwa amelazwa katika kitengo cha ICU cha hospitali ya Nairobi alipofariki mwendo wa saa tatu usiku wa Jumatatu.

Huku akimuomboleza marehemu Jahmby siku ya Jumanne mchana, Mbusii alimtaja kama rafiki yake na kuitaka roho yake ipumzike kwa amani.

“Pumzika vyema rafiki yangu. Mpaka tukutane tena, angaza njia yako,” Mbusii alimuomboleza Njambi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Marehemu Njambi ambaye alijulikana kwa kupenda reggae huku akitangaza baadhi ya vipindi vya redio na televisheni alikuwa ametatizika kwa takriban miongo miwili kutokana na ugonjwa wa endometriosis.

Mbunge Phelix Odiwour almaarufu Jalang’o ametambua vita vikali vya Njambi na ugonjwa huo na kutaka roho yake ipumzike kwa amani.

“Ulipigana! Kama marafiki tulifanya bidii yetu, mbingu imeshinda moyo wa dhahabu! Pumzika salama jamani! Hii inauma!,” Jalang’o alisema.

Wafuatao ni baadhi ya mastaa wengine waliomuomboleza marehemu Jahmby:

Blessed Njugush: Mpiganaji amepumzika. Roho yake ipumzike kwa Amani. Alitufundisha uthabiti, Imani ya nguvu, Tumaini na Fadhili. Muda mrefu sana Fire Mummah.Pole kwa familia na marafiki.

Betty Kyallo: Pambano lako lilikuwa la kushangaza kweli. Mwanajeshi wa kweli. Vita vyako viliufanya ugonjwa huu ujulikane. Nina hakika wanawake wengi ambao hawakujua kuhusu hilo na walikuwa wakiteseka hatimaye walikuja kuelewa kuhusu hilo na pia kupata msaada wa matibabu. Bingwa wa kweli. Mbinguni ikupokee kwa faraja unayostahili.

Ken Mijungu: Tumempoteza shujaa. Njambi alipoteza pambano alilopigana kwa ujasiri hadharani na faraghani. Alikuwa binadamu mzuri! RIP rafiki yangu

Suzanna Owiyo: Roho nzuri imepumzika. Nenda vizuri Njambi Koikai aka Fyah Mama

Sauti Sol: Siku ya Huzuni 💔💔💔 Milele mioyoni mwetu. @jahmbykoikai alikuwa meneja wetu wa kwanza kabisa. Alichukua sehemu kubwa katika hatua zetu za awali kama bendi. Sekta imepoteza thamani. Nchi imepoteza shujaa. Mbingu zimepata malaika. Pumzika kwa Nguvu. Roho yako inaishi milele!

Shix Kapyenga: Hii imeuma 💔Rest In Power Fyah Mama

Mwalimu Churchill: Rest in Power @jahmbykoikai .Umepambana vyema.