Mambo yasiyojulikana sana kuhusu mamake Diana Marua yaibuka kwenye video ya kaburi lake (+picha)

Mamake Diana alikuwa na umri wa miaka 40 tu wakati alipofariki.

Muhtasari

•Diana aliashiria kujivunia mafanikio yao makubwa na hata ‘akazungumza’ na marehemu mama yake kuhusu hilo akimwambia kwamba anatumai pia yeye anajivunia yeye.

•Msalaba kwenye kaburi hilo una maandishi yanayofichua kwamba mamake Diana alijulikana kama ‘Lilian Nyambura Gikurumi’. 

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Siku ya Jumatano, wapenzi maarufu wa Kenya Bahati na Diana Marua walionyesha kionjo cha Reality Show yao mpya ‘The Bahati’s Empire’ ambayo itaonyeshwa kwenye Netflix.

Diana aliashiria kujivunia mafanikio yao makubwa na hata ‘akazungumza’ na marehemu mama yake kuhusu hilo akimwambia kwamba anatumai pia yeye anajivunia yeye.

"Mama, tumefanikiwa. Natumai unajivunia mimi huku ukitazama kutoka mbinguni,” Diana aliandika chini ya video ya kionjo ambayo aliichapisha kwenye Instagram.

Katika video hiyo, mama huyo wa watoto watatu alisikika akizungumza kuhusu kukua bila mama yake na akaeleza jinsi anavyotamani angekuwepo kuwalea.

“Nyakati nyingine huwa natamani mama yangu angekuwapo nilipokuwa nakua,” alisema.

Video hiyo pia iliangazia mahali maalum ambapo marehemu mama ya Diana alizikwa miaka mingi iliyopita. Kaburi lake liko kwenye shamba kubwa kijijini.

Msalaba kwenye kaburi hilo una maandishi yanayofichua kwamba mamake Diana alijulikana kama ‘Lilian Nyambura Gikurumi’. Alizaliwa Aprili 1969, na kufariki Machi 2009. Alikuwa na umri wa miaka 40 tu wakati alipofariki.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwezi uliopita, mke huyo wa mwimbaji Kelvin Bahati alimwandikia marehemu mamake barua ya wazi alipokuwa akimkumbuka na kumuenzi.

Marua alitumia mitandao ya kijamii kushiriki ujumbe wa dhati kwa mamake, akimfahamisha jinsi yeye na familia yake wanavyoendelea tangu alipoaga..

Alisema anatamani mama yake angekuwapo ili kushuhudia mafanikio yote aliyoyapata katika umri wake.

 Hii hapa barua ya Diana Marua kwa mama yake;

Mama mpendwa,

Nakumbuka matendo yako mema mara nyingi sana    Laiti ungalikuwa hai leo, Mungu anajua ni kiasi gani ningekufanyia. Ninakaa na kujiuliza maisha yangekuwa tofauti na wewe karibu, lakini Mungu alikuwa na mipango mingine ambayo siwezi kuhoji 🙏🏼

Labda ningekununulia magari, labda ningekununulia vito vya thamani kwa sababu ulivipenda sana, labda leo ... ningekushangaza kwa kipande cha ardhi au labda msimu huu wa Siku ya Kina Mama, ningekuwa nikifumba macho kukushangaza kwa nyumba ya kifahari yenye samani lakini tena, ninachoweza Kusema ni, Asante Mungu kwa kuniruhusu kushiriki miaka michache niliyokaa nawe 😭

Nimesalia kutunza kumbukumbu ninazounda na watoto wangu kila siku. Lengo langu ni kuwapa maisha ambayo sikuwahi kuwa nayo, nikitumaini kwamba wanapokua, watathamini wakati wetu pamoja.

Mama, najua wewe ni Malaika mlezi wangu, nilichosema kwenye video ya leo…. Ni barua kwako, natumai nimekufanya ujivunie kuwa Msukumo kwa Kizazi changu 🙏🏼