logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waihiga Mwaura aadhimisha miaka 40 kwa kumshukuru mkewe

Ninaingia katika miaka 40. Nimebarikiwa kufikia hatua hii muhimu Mungu anaendelea kuwa mwaminifu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 June 2024 - 12:14

Muhtasari


  • •Mwanahabari Waihiga Mwaura ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 40 leo Alhamisi, Juni 6.
  • •Mwanahabari huyo alitoa shukrani kwa mke wake mpendwa, Joyce Omondi, kwa usaidizi wake usioyumba.
  • •Joyce pia alikwenda kwenye sehemu ya maoni kumsifu, akielezea mtangazaji wa habari kama zawadi ya ajabu.

Mwanahabari mashuhuri Waihiga Mwaura ameadhimisha hatua muhimu maishani mwake kwa kufikisha umri wa miaka 40.

Mwandishi huyo wa BBC aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mnamo Alhamisi, Juni 6.

Waihiga alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kusherehekea siku yake na wale ambao wamechangia mafanikio yake.

Alimpongeza mkewe, Joyce Omondi, kwa msaada wake.

"Ninaingia katika miaka 40. Nimebarikiwa kufikia hatua hii muhimu Mungu anaendelea kuwa mwaminifu.

Ninamshukuru mke wangu, @joyceomondi, familia na marafiki, ambao wamefanya safari hiyo kuwa ya kuridhisha kufikia sasa. Ninashukuru kwa yaliyopita na ninafurahiya siku zijazo," aliandika.

Mtangazaji wa zamani wa Citizen TV alimalizia ujumbe wake kwa mstari wa Biblia kutoka katika Isaya 40:31:

 “Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia."

Joyce alijibu chapisho hilo kwa shauku, akithibitisha upendo wake usioisha kwa Wahiga.

"Siku ya kuzaliwa yenye furaha zaidi, mpenzi wangu! Wewe ni zawadi ya ajabu sio kwangu tu na familia yetu bali pia kwa vizazi vinavyokuzunguka na ulimwengu wote. Mazuri yako ndio mwanzo tu! Aheri muno," Joyce aliandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved