logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kitinda-mimba amlilia boyfriend wake kumuoa haraka ili kumuokoa dhidi ya kuendelea na masomo

Ni tabia zipi ambazo unazioata za kukera kutoka kwa watoto ambao ni wa mwisho kuzaliwa katika familia?

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 June 2024 - 08:52

Muhtasari


  • • Kwa mujibu wake, kuendelea na masomo ni jambo gumu sana na ambalo hawezi kulikwepa isipokuwa tu kuitorokea ndoa.

Ni hadithi zipi ambazo unazisikia zinahusishwa na watoto haswa wale wa kike ambao ndio vitinda mimba katika familia zao?

Kijana mmoja katika mtandao wa TikTok ameshiriki uzoefu wake kutokana na kuchumbiana na mwanamke ambaye ndiye kitinda mimba kwao.

Kijana huyo alipakia video wakiwa na mpenzi huyo wake ambaye ni kitinda mimba katika familia yao, na kuonyesha jinsi anataabika kumlea kimapenzi, akilazimika kumhendo kwa utaratibu na umakini mkubwa kama yai ili asije akamkera na kumuudhi.

Kwa kawaida, watoto vitinda mimba katika familia hudekezwa kwa mtindo wa kipekee, muda wote wakichukuliwa kuwa na akili za kitoto hata kama wameshakomaa na kuwa watu wazima.

Katika video hiyo, mrembo huyo ambaye kwa muonekano ni mwanafunzi wa masomo ya baada ya sekondari alionekana akimuomba na kumsihi mpenzi wake kufanya haraka ili kufika kwao na kumlipia mahari kama njia moja ya kuhakikisha amemnasua kutoka kwa ‘janga’ la kuendelea na masomo.

Kwa mujibu wake, kuendelea na masomo ni jambo gumu sana na ambalo hawezi kulikwepa isipokuwa tu kuitorokea ndoa.

Katika sehemu ya video hiyo, mwanadada huyo alionekana akiwa na wakati mzuri zaidi tofauti na alipokuwa akitokwa na machozi katika sehemu nyingine kuhusu kurejea shuleni.

"Njoo ulipe malipo kwa wazazi wangu ili nisiende shule tena," alisema.

 

Tazama video hapa chini…


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved