Mtayarishaji maudhui kutoka Kenya Crazy Kennar amefichua anachofanya nchini Afrika Kusini
Akizungumza katika mahojiano na Mungai Eve, Crazy Kennar alisema aliamua kuhamia Afrika Kusini ili kujifunza zaidi na kupata ujuzi zaidi kuhusu filamu.
“Nchini Afrika Kusini kwa sasa ninasomea uandishi wa filamu, mimi ni content creator nilianza kama mwigizaji, mimi nilizaliwa kama mwigizaji lakini kuna ujuzi nilipata njiani," alieleza.
Kennar anasema kuwa uamuzi wake wa kurejea shuleni pia umechangiwa na kutimiza ndoto yake ya kushinda tuzo ya Oscar na hiyo inamtaka aongeze maarifa zaidi na hiyo inahusisha yeye kufanya mambo zaidi ambayo ndiyo anafanya.
“Lakini tukisonga songa kuna kitu kinaitwa ceiling board na kwako kukua zaidi ya ceiling board ni ukue na resources, knowledge ama kitu inaitwa patronage na mimi point imefika kuna concept naandika na ndio niongeze size ya ndoto zangu lazima nifanye mambo kupita kwaida.”
Kennar anaamini kuwa anafanya kazi kwa kizazi cha sasa na hiyo ndio sababu kuu ya kuongeza maarifa.
Crazy Kennar alisema kuwa alifanya hivyo kwa sababu ana mpango wa kuendelea na masomo zaidi.
"Kiwango kipya kimefunguliwa. Safiri pamoja nami ninaposhiriki maisha yangu na wewe kama mbunifu mahiri wa Kenya anayesoma Afrika Kusini, anayeishi Kenya na Afrika Kusini huku akitengeneza maudhui kote ulimwenguni.” Crazy Kennar alieleza.
Kennar alieleza kuwa hio ni hatua chanya kwa maendeleo yake ya kibinafsi na kitaaluma, kwani kusoma nje ya nchi kunaweza kutoa mitazamo tofauti katika kazi yake.