Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Vera Sidika amefichua kuwa bado alikuwa kijana mdogo wakati alipotengenezea shilingi milioni moja.
Wakati kiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram siku ya Jumatano, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 34 alifichua kwamba alipata kiasi hicho cha pesa akiwa na umri wa miaka 19 pekee.
"Ulipotengeneza milioni yako ya kwanza, ulikuwa na umri gani," mwanamtandao alimuuliza.
Vera alijibu, "Umri wa miaka 19."
Mwanamtandao mwingine alitaka kujua saizi yake makalio yake na alisema, "inchi 60."
Katika majibu yake, mama huyo wa watoto wawili pia alithibitisha kuwa yuko kwenye uhusiano na mwanamume kutoka Nigeria, ambako sasa yuko.
"Habari za asubuhi kwa mpenzi wa maisha yangu. Walimwengu wengine wanaweza kusalimiana. Lagos,” aliandika.
Siku chache zilizopita, mwanasoshalaiti huyo aliyezingirwa na drama aliwaacha wengi katika hali ya mshangao baada ya kuandaa tafrija kubwa kwa ajili tu ya kusherehekea kuvunjika kwa ndoa yake mwezi Septemba mwaka jana.
Sidika kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia mfululizo wa picha na video akionyesha jinsi aliwasili katika tafrija hilo kubwa aliambatanisha na ujumbe mkuu kuhusu tafrija hilo.
Sidika ambaye alikuwa ameoleka kwa msanii Brown Mauzo kwa kipindi cha miaka 3 na kupata watoto wawili pamoja aliwataarifu mashabiki wake kwamba ameamua kuandaa bonge la tafrija kusherehekea kuvunjika kwa ndoa, akisema ndoa ni utapeli mkubwa sana kuwahi kutokea katika maisha yake.
“Tafrija ya kusherehekea talaka inakuja, ndoa ni utapeli,” aliandika Sidika kwenye insta story yake.
Mama huyo wa watoto wawili – Asia Brown na Ice Brown – alionekana akishuka kwenye gari bichi nyakati za usiku huku amezingirwa na mabaunsa na kuzindikizwa kwenye ukumbi mkuu kulikoandaliwa tafrija hiyo.
Mapema mwezi jana, Sidika katika mahojiano alisema kwamba jambo linalomfurahisha Zaidi na mwaka huu kuelekea kipindi cha majira ya joto ni kwamba hana mimba wala hayuko katika ndoa, hivyo atapata muda mzuri Zaidi wa kujirusha kwa raha za kila aina.
Alisema kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamume raia wa Nigeria lakini akasema kuwa si uhusiano ambao anaweza sema ni ule wa kumwajibisha sana kwani yuko mguu mmoja ndani na mguu mwingine nje.
Mjasiriamali huyo alisema hatarajii kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi ambao utamfungia kwa majukumu kwani anataka muda wake wa kujirusha na pia kama ni kupata mtoto basi ni baada ya kama miaka 7 hivi ijayo, wala si wakati wowote hivi karibuni.