Siku ya Jumanne, aliyekuwa gavana wa Nairobi Gideon Mbuvi almaarufu Mike Sonko alibadilishana mazungumzo na baadhi ya wafuasi wake kwenye mtandao wa X kufuatia kurejea kwa binti yake Sandra Mbuvi almaarufu Thicky Sandra.
Mfanyibiashara huyo tajiri alikuwa ametumia mtandao huo wa kijamii kuwafahamisha wafuasi wake kuhusu kurejea kwa bintiye mrembo ambaye amekuwa akiishi Ulaya.
Sonko alifichua kuwa mwanadada huyo alitua nchini siku ya Jumanne asubuhi na atakaa nchini kwa mapumziko marefu ya msimu wa joto.
"Nimempokea hivi punde binti yangu Sandra, ambaye alirejea kutoka London asubuhi ya leo kwa mapumziko marefu ya msimu wa joto. Karibu tena. Tuliku’miss sana,” Sonko aliandika chini ya video akimkaribisha Sandra katika uwanja wa ndege.
Katika video hiyo, mrembo huyo alionekana kuwezwa na hisia kuungana tena na familia yake nchini Kenya kabla ya kusindikizwa nyumbani kwa magari ya kifahari.
Mamia ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walikusanyika chini ya chapisho la Sonko ili kusaidia katika kumkaribisha Sandra nchini na kutoa maoni mengine. Baadhi ya watumiaji wa mitandao hata waliendelea zaidi kutangaza mapenzi yao kwa mrembo huyo, na hivyo kuibua majibu makali kutoka kwa gavana huyo wa zamani wa Nairobi.
"Ninampenda, asante kwa kuwa baba mzuri," Felix aliandika kwenye chapisho la Mike Sonko.
Huku akimjibu, mwanasiasa huyo anayezingirwa na utata mwingi alisema, “Asante. Lakini huyu mpaka amalize kusoma unless unataka nikulipue sehemu ny*ti.”
Mtumiaji mwingine wa X, BuseneM alisema, “Mheshi, nitakuja kuchumbia huyu mrembo. Natumai mkwe wangu.”
Sonko akajibu, “Lazima amalize masomo fala hii.”
Boniface Kisina alisema, "Umenyima mpenzi wake nafasi ya kulaki dem wake sasa."
Akajibu, “Ungekuja ukule nyahunyo ya matako.”
Mapema mwaka huu, binti huyo mdogo zaidi wa Sonko alidai kwamba madai yake ya mahari yanajumuisha vitu kama vile Simba na Bentleys.
Mrembo huyo kwenye Instastori zake, aliwafahamisha mashabiki wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kuhusu mamilioni ya pesa ambazo mumewe mtarajiwa atalazimika kutoa ili kufunga ndoa naye.
"Wazazi wangu wanataka simba watano 3 chopa 22 Bentley, rover 4, na pauni milioni 500 (Sh87,476,366,250)," alisema.