Mfanyibiashara wa Uganda Shakib Cham Lutaaya, mume wa mwanasosholaiti Zari Hassan, ameamua kuuonyesha ulimwengu ndugu zake watatu.
Siku ya Alhamisi, kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 alishiriki picha zake nzuri akiwa na dada zake wadogo wawili na nyingine akiwa na kakake mdogo.
Katika posti hizo alizochapisha kwenye Instagram, pia alifichua jinsi dada zake wanavyojitambulisha kwenye mtandao huo wa kijamii ambapo mmoja anajitambulisha kuwa ni @sltaaya na mwingine @hot_l_s.
Kaka wa mfanyabiashara, kulingana na picha aliyoshiriki ni mdogo kuliko yeye na dada. Walakini, wanafanana sana.
Hakuna mengi yanayojulikana kuhusu familia ya Shakib Lutaaya. Hata hivyo amemuonyesha mamake hadharani siku za nyuma alipokuwa akimsherehekea.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, Shakib alimsherehekea mama yake wakati ulimwengu mzima ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Mume huyo wa Zari Hassan alishiriki video nzuri ya kumbukumbu yake na mama yake katika hoteli ya kifahari ambapo alikuwa amempeleka mzazi huyo kwa likizo.
Katika sehemu ya maelezo ya video hiyo aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram, Shakib alimsherehekea mzazi huyo wake na kutumia fursa hiyo kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.
"Kheri ya siku ya kuzaliwa Hajat.. Nakupenda," Shakib aliandika chini ya video hiyo ya kupendeza.
Hajat katika Uislamu maana yake ni "kutamani."
Katika picha hiyo, mamake Shakib alionekana akiwa amevalia mavazi mekundu na alionekana kufurahishwa sana na likizo hiyo. Alionekana mwenye afya njema na mwenye nguvu.
Shakib alizaliwa jijini Kampala, Uganda mwezi Desemba 1992 na kukulia huko kabla ya kuhamia Afrika Kusini baadaye maishani kwa ajili ya kutafuta riziki. Ni maelezo kidogo kuhusu familia yake, historia yake na maisha ya kibinafsi yanajulikana.
Zari Hassan pia alizaliwa nchini Uganda katika mji wa Jinja kwa wazazi wa Uganda Nasur na Halima Hassan. Babu yake mzaa mama ni Mhindi ilhali nyanya yake anatoka Uganda, pengine sababu ya yeye kuwa na ngozi nyeupe kwa kiwango.
Wapenzi hao walikutana nchini Afrika Kusini miaka kadhaa iliyopita, wakachumbiana kwa muda kabla ya kutengana na baadaye kuungana tena mwaka wa 2022. Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu katika harusi ya Kiislamu (Nikah) mwezi Aprili mwaka jana kabla ya kufunga ndoa rasmi Oktoba.