Mtangazaji wa habari maarufu wa Kenya Betty Mutei Kyallo hatimaye amefichua sura yaa mpenzi wake mpya.
Mtangazaji huyo mrembo alichukua hatua hiyo usiku wa kuamkia Ijumaa wakati akimsherehekea mpenzi wake mnamo siku yake ya kuzaliwa.
Katika ujumbe wake kwa mpenzi wake, Betty Kyallo alimtakia mambo mema na kwa uhusiano wao.
"Heri ya kuzaliwa mpenzi. Vicheko zaidi, furaha zaidi, kukumbatiana zaidi, watoto zaidi, sisi zaidi. Ni hivi,” Betty Kyallo aliandika kwenye mtandao wa Instagram.
Aliambatanisha ujumbe wake na picha nzuri yake na mwanaume huyo. Pichani, mwanamume huyo anaonekana kuwa mrefu zaidi na ana rasta kichwani.
Mama huyo wa binti mmoja aliendelea kumshukuru mpenzi wake na kusherehekea mapenzi yao.
"Asante kwa kila kitu. Heri ya kuzaliwa,” aliandika.
Kyallo alijigamba kwa kujipatia mwanamume anayefaa na kuwapuuza kila mtu mwingine.
“Mungu alinitumia aliye sahihi. Nyinyi nyote mnaweza kuwa na hasira,” alisema.
Pia alijigamba kuhusu kuwa na furaha na mpenzi wake mpya na kumtakia mwanaume huyo mafanikio zaidi.
"Naomba mtu wangu ashinde kila wakati. Anashinda lakini nataka ashinde mengi zaidi. Juu ya Mungu. Furaha mke, maisha ya furaha,” alisema.
Hatua hiyo ya mtangazaji huyo mrembo imezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya wanamtandao wakiwapongeza na kuwatakia kila la heri huku wengine wakiibua madai kuwa mwanamume huyo ni mdogo sana kwa Kyallo.
Huku akijibu madai ya mpenzi wake kuwa na umri mdogo sana kuliko yeye, mama huyo wa binti mmoja alisema, "Hata hivyo, angalau miaka imeongezeka. Nina furaha. Wacha tusukume. Mambo ni deadly deadly.”
Mapema mwaka jana, mtangazaji huyo wa habari wa zamani alidokeza kwamba ni wakati sasa anahitaji kupata mtoto wa pili.
Katika mahojiano na wanablogu, Betty Kyallo alisema kwamba mtoto wake wa kwanza ambaye alizaa na mwanahabari mwenzake Dennis Okari kabla ya kutengana amekuwa akimpa shinikizo la kutaka ndugu.
Mwanahabari huyo alisema atang’ang’ana safari hii na kupunguza shinikizo hilo kwa kumzalia kifungua mimba wake ndugu.
“Kusema kweli ndio, nafikiri ni muda wa kufikiria kuongeza familia, mtoto. Ivana amekuwa akinipa shinikizo la kutaka dada, kaka. Nafikiri anahitaji mtu wa kumpa ushirikiano, nitamtafutia, nitang’ang’ana,” Kyallo alisema.