Katika mahojiano ya hivi majuzi, wanandoa Nimo na Mr. Seed walitoa muhtasari wa uhusiano wao wa kudumu.
Mazungumzo hayo yalihusu maamuzi ya zamani ya Nimo ya kuondoka kwenye ndoa, na hatimaye kurejea na kuendelea na uhusiano wao nguvu zaidi.
Mr Seed alimuliza mkewe moja kwa moja kuhusu utengano wao wa mara kwa mara, na kusababisha jibu la upendo kutoka kwa Nimo.
Alifafanua katika uhusiano wao wamepitia mengi kama familia lakini kupitia uzoefu wao pamoja kwa karibu muongo mmoja bado wako pamoja.
"Tumepitia mengi pamoja kwa kweli wewe ni familia," alisema.
Nimo alikubali jukumu muhimu la Mr Seed katika utulivu wa familia yao na pia wajibu wake wa kifedha na kujitolea kama baba mzazi.
“Unafanya mambo ambayo wengi hawangefanya na ninakupenda jinsi ulivyo,” Nimo alisema.
Nimo pia alitoa shukrani kwa msaada usioyumba wa Mr. Seed hasa katika nyakati ngumu. “Tumekabili magumu lakini hukati tamaa kamwe. Daima unapigania uhusiano wetu,”Nimo alikiri.
Nimo alithamini sana kuendelea kwa Mr Seed kutafuta njia za kuungana tena baada yake kuondoka katika ndoa.
“Si kila mtu anakufuata baada ya kutoka lakini wewe ukuniacha,” Nimo alikiri.
Mr. Seed, kwa upande wake, alionyesha shukrani zake kwa upendo wa Nimo na usaidizi usioyumbayumba.
"Kuwa na wewe kando yangu,na kuonyesha upendo kwangu na familia yangu, kunamaanisha ulimwengu," Mr Seed alisema.