Mcheshi wa Kenya na MwanaYouTube Oga Obinna ameeleza ni kwa nini alikosa uzinduzi wa licha ya kuwa alialikwa.
Obinna, ambaye alikuwa akizungumza katika kipindi chake cha kawaida cha kila wiki cha YouTube, alisema sababu ni kwamba aliarifiwa wakati ukiwa umeenda kama siku moja kabla, na tayari alikuwa amefanya mipango ya siku hio.
“Sikuweza kufika kwa ajili ya uzinduzi siku hiyo kwa sababu, nilikuwa na kazi,mwaliko ulikuja siku moja kabla na siku yangu nilikuwa nimepanga.” Obinna alisema.
Sababu nyingine ilikuwa ni kwa sababu alikuwa anamalizia kupiga show yake mpya, ‘My Woman Ke’ ambayo alisema inaonyeshwa kwenye chaneli yake ya YouTube.
Akieleza kuwa anachojaribu kufanya katika kipindi hicho kipya ni kutafuta mwanamke.
Hata hivyo, aliwapongeza wawili hao kwa kuwa wanandoa wa kwanza Wakenya kuachilia onyesho la ukweli lililoonyeshwa kwenye Netflix.
“Hongereni sana, Diana na Bahati; kwa kawaida huitwa checkmate, na hatua hiyo ni nzuri sana Netflix—hilo ni jambo kubwa.
Ni sawa kila mtu kusherehekea. Nyinyi sio waandishi tu bali waigizaji, na mnaimiliki vitu vizuri. Hongera sana endelea kushinda. Napenda vijana wanaposhinda.” Obinna alisema.