logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arrow Bwoy aeleza sababu za kutaka Nadia amruhusu kuoa mke mwingine

Arrow Bwoy pia alieleza kuwa anapanga kuoa mke mwingine kwa sababu dini yake inamruhusu kufanya hivyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 June 2024 - 12:30

Muhtasari


  • •Arrow Bwoy pia alieleza kuwa anapanga kuoa mke mwingine kwa sababu dini yake inamruhusu kufanya hivyo.
  • •Alidokeza kuwa anataka watoto zaidi, na ikitokea mke wake hataki kumuongeza zaidi, basi amruhusu alete mke mwingine pamoja naye.

Msanii wa Kenya Arrow Bwoy amefichua sababu inayomfanya afikirie kuoa mke wa pili, iwapo mke wake atamruhusu kufanya hivyo.

Arrow Bwoy ambaye alikuwa kwenye mahojiano na Obinna TV, alidokeza kuwa anataka watoto zaidi, na ikitokea mke wake hataki kumuongeza zaidi, basi anaomba amruhusu alete mke mwingine pamoja naye.

Sababu inayomfanya atamani kuwa na watoto wengi zaidi ni kwa sababu anahisi kwamba mtoto wao wa pekee, ambaye ni mvulana  amekuwa mkubwa, na anafikiri akiwa na ushirika na watoto wengine sio wazo mbaya.

“Jambo moja ambalo nina tatizo nalo ni mtoi wetu amefika karibu miaka 2 na 3, hivyo nataka pia mbogi nataka niongeze lakini amekaza.

 Alafu pia, she is a baby girl nataka akue forever a baby girl the way she is na sitaki pia asumbuke sana ndio nimemwambia nitafute mtu mwingine juu yangu aim yangu nataka watoto watatu,” Arrow Bwoy alisema.

Arrow Bwoy pia alieleza kuwa anapanga kuoa mke mwingine kwa sababu dini yake inamruhusu kufanya hivyo.

“Kikwetu tunakubaliwa mimi ni muslim, jina yangu ni Ali, so mimi naomba anipe ruhusa nichukue dem mwingine, but bado, I will retain her, of course, my baby girl forever.

 Nataka bibi mwingine tupate watoto wawili na ni hivo. Arrow Bwoy alisema.

Nadia na Arrow Bwoy walipata mtoto wao wa kwanza pamoja, mtoto wa kiume, mnamo Machi 24, 2022.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved