logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa ajitosa mitandaoni kumtafutia dada wa mkewe mume baada ya kufuzu mafunzo ya NYS

Alisema hana uhakika na ubikira wake baada ya kuenda NYS.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 June 2024 - 08:12

Muhtasari


  • • Pia alimtaja kwa jina lake halisi analolitumia Facebook pamoja na kuambatanisha na namba yake ya simu kwa ajili ya wanaum kujaribu bahati yao kumtongoza.

Mwanamume mmoja amezua gumzo katka mtandao wa Facebook baada ya kuchapisha tungo refu akimnadi shemeji yake kwa lengo la kumtafutia mwanamume wa kumuoa.

Mtu huyo kwa jina Prince Ozed kwenye Facebook alisema kwamba dada mdogo wa mkewe alikuwa anaishi naye na baada ya kuenda katika mafunzo ya NYS na kufuzu, alihitaji kumtafutia mume ili kuondoka katika nyumba yake.

Ozed alisema kwamba dada huyo wa mkewe alikuwa anaishi nao na alikuwa bikira lakini akasema baada ya kwenda NYS na kumaliza, hawezi kulihakiki hilo la ubikira lakini akamsifia kuwa ni binti mzuri ambaye yuko tayari kuoleka.

“Ikiwa unatafuta Mtoto wa Onicha kuoa, Huyu amefuzu leo. Anawajibika na anafanya kazi kwa bidii. Alikuwa bikira alipotoka nyumbani kwenda kwenye huduma ya NYS lakini baada ya kutumikia, siwezi kuthibitisha hilo tena. Yeye ni Introvert. Yeye hana kichefuchefu sana. Mambo madogo ndio yanamfanya kulia. Yeye ni stylist (anatengeneza Nywele),” Ozed alimsifia shemeji yake.

Alisema kwamba binti huyo yuko tayari muda wowote kuolewa na mwanamume atayayejitokeza, akisema kuwa hata yeye kama shemeji angependa kuona hilo likitokea kwani ana njaa ya wali pilau na mapochopocho mengine kwenye harusi.

Pia alimtaja kwa jina lake halisi analolitumia Facebook pamoja na kuambatanisha na namba yake ya simu kwa ajili ya wanaum kujaribu bahati yao kumtongoza.

“Ukimpigia simu na uzungumze naye vizuri, anafaa kuja moja kwa moja hadi nyumbani kwako na kutoka nyumbani kwako hadi kijijini kwao, hakuna wakati wa kupoteza, Wali wa harusi unanipa njaa kweli,” Ozed alisema.

Akifuatilia chapisho hilo, binti huyo alisema kwamba tayari alikuwa amepokea simu kadhaa kutoka kwa wanaume, muda mchache baada ya shemeji yake kuweka wazi namba yake.

“Kuhusu post aliyotoa shemeji yangu Prince Ozed nimepokea simu zisizopungua 20 na bado nahesabu na dm yangu imejaa tayari kama sijajibu usikasirike nimekuwa busy.”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved