Mwanamuziki aliyesainiwa na Diamond Platnumz, Zuchu amejawa na furaha baada ya mkali wa RnB kutoka Marekani, Chris Brown kufanya changamoto ya kucheza kwenye wimbo wa mwimbaji wa Tanzania 'Komasava' (Comment Ca Va).
Katika ujumbe wake, Zuchu alisema kutambuliwa huku ni jambo kubwa.
Aidha msanii huyo alisema kwamba bendera ya tasnia ya Tanzania imepeperushwa duniani.
Zuchu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia video ya mwimbaji huyo( Chris Brown) akifanya challenge.
"Hatuwezi jifanya kwamba hili sio jambo kubwa. Kwa kweli hili ni jambo kubwa sio tu kwa diamond platnums bali kwa taifa zima la uswahilini na Afrika kwa ujumla.Bendera ya Tasnia leo Imepeperushwa @diamondplatnumz Azidi kufanya taifa litembee kifua. mbele."
Aliendelea na ujumbe wake na kusema;
"Komasavaa to the world @chrisbrownofficial taifa letu Na Afrika kwa ujumla siku zote itakuheshimu kwa Kuwakilisha utamaduni kwa uzuri sana MR BROWN .MUDA WETU UNAFIKA 🇹🇿❤️."
Katika wimbo huo, Diamond Platnumz aliwashirikisha Khalil Harisson na Chley. Video ya wimbo huo imetazamwa zaidi ya milioni 2.7 kwenye Youtube.