Gavana wa zamani wa Oparanya Wycliffe Oparanya kwa mara ya kwanza amezungumza ni kwa nini hakuaibika kuhusu kuwa na mpenzi, kipusa mdogo baada ya picha zake na mrembo huyo kuvujishwa mitandaoni miezi michache iliyopita.
Akizungumza kwenye runinga ya KTN Home, Oparanya alisema kuwa yule ni mpenzi wake na hana lolote la kuficha au kukana kuhusu hilo kwa sababu yeye ndiye humhudumia.
Mwanachama huyo wa ODM alisema kuwa mrembo huyo huja nyumbani kwake mara kwa mara hata wakati wake zake wawili wako, na wake zake huwa hawaoni vibaya kwa sababu anatimiza mahitaji yao ipasavyo.
Oparanya alisema kuwa yeye huwa mkweli na ni kitu ambacho alifunzwa na marehemu mamake, hivyo hawezi kukwepa jambo lolote linalomlenga na ambalo ni la kweli.
“Mimi nina wake 2 na pia nina ‘girlfriend’ na mimi sina shida hata na mke wangu hapa. Hata girlfriend wangu huja hapa na mke wangu hana tatizo na hilo kwa sababu huwa ninamhudumia vizuri.”
“Unajua mimi kama ambavyo nimekwambia nilizaliwa kama mtoto wa pekee kwenye familia yetu, hivyo mamangu alinifunza kuwa mkweli (Kiuhalisia tulizaliwa 5 lakini kwa bahati mbaya wazawa wa kwanza 4 walikufa na nikawa pekee niliyesalimika). Na kwa sababu nilizaliwa peke yangu, mamangu angeniambia kila mara, ‘mwanangu, ni kwa bahati mbaya kwamba ulizaliwa peke yako hivyo ukikua pata watoto wengi ili kunilipizia wale ambao ningepata mimi’. Na hivyo ndivyo nimekuja kuwa mkweli,” Oparanya alieleza.
Kuhusu mpenzi wake mpya na ni nani aliyevujisha picha zao, Oparanya alisema;
“Unajua baada ya siasa, unahitaji mtu wa kuku’keep busy. Unajua mke wangu sasa yuko hapa lakini hawezi tembea na mimi kwenda kila mahali, wakati mwingine unahitaji tu ku’relax na msichana mrembo kando yako. Ndio maana nikamchagua. Sikuwa na shida hata kidogo kuhusu picha kusambaa mitandaoni, mimi niko tu sawa na ndio maana nikazungumzia tukio lile.”
“Hata hivyo, hakuna nafasi ya mrembo mwingine tena kwa maisha yangu, maisha ya sasa hivi yamekuwa ghali. Mimi nina wake wawili, mmoja yuko hapa [Butere] na mwingine yuko Likuyani. Kuwa na wake wawili ni kitu tu kilitokea, kitu ambacho huwezi pangia. Lakini pia nilikuwa natilia maanani ushauri wa mamangu.”