logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dorea Chege aeleza sababu za kutokuwa tayari kuzaa

Dorea Chege alisema kuwa kupata mtoto ni uamuzi wa hiari, na hatazaa tu kwa sababu watu wanamtaka.

image
na Davis Ojiambo

Burudani26 June 2024 - 07:50

Muhtasari


  • •Dorea Chege alisema kuwa kupata mtoto ni uamuzi wa hiari, na hatazaa tu kwa sababu watu wanamtaka, na kusisitiza kwamba atapata mtoto akiwa tayari.
  • •Dorea Chege na mpenzi wake,DJ Dibul , wamekuwa pamoja kwa muda lakini bado awajaliwa na mtoto.

Sosholaiti Mkenya na mwigizaji wa zamani wa Maria Dorea Chege ameeleza sababu inayomfanya hafikirii kupata watoto kwa sasa.

Dorea Chege alisema kuwa kupata mtoto ni uamuzi wa hiari, na hatazaa tu kwa sababu watu wanamtaka, na kusisitiza kwamba atapata mtoto akiwa tayari.

“Ni kwa sababu moja, hakuna mtu ananilazimisha kupata mtoto na mimi sipelekanangi na shinikizo la rika la watu."

"Nitapata mtoto nitakapohisi niko tayari.” Dorea Chege alisema.

Alieleza kwa kutoa mambo matatu ambayo yatamfanya apate mimba ambayo ni wakati anapokuwa na utulivu wa kimwili, kihisia, na kifedha.

"Lazima niwe na utulivu wa kifedha na utulivu wa kihisia kwa sababu mtoto huyo anahitaji mama wa aina hiyo," alisema.

Dorea Chege ambaye alipata jina lake la utani ‘Maggie’ alipokuwa mhusika kwenye kipindi cha Maria, kwa sasa amechumbiwa na Dj Dibul.

Wawili hao hawajawahi kukwepa kutangaza mapenzi yao hadharani.

Dorea Chege na mpenzi wake,DJ Dibul , wamekuwa pamoja kwa muda lakini bado awajaliwa na mtoto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved