logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eric Omondi alia kwa huzuni wakati wa ibada ya wafu kwa marehemu kakake, Fred Omondi

Frd Omondi alifariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wiki mbili zilizopita.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 June 2024 - 06:53

Muhtasari


  • • Alikuwa ni mdogo wake Eric Omondi, na kaka wa pekee aliyekuwa amesalia kwa Eric baada ya kaka yao mwingine kufariki mwaka 2018.
  •  
ERIC OMONDI AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI VWA IBADA YA WAFU YA KAKA YAKE

Mchekeshaji aliyegeuka na kuwa mwanaharakati Eric Omondi na mpenziwe Lynne Njihia wamewasili katika makafani ya Chiromo asubuhi ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya safari ya mwisho na marehemu mdogo wake, Fred Omondi.

 Ibada ya wafu iliandaliwa katika makafani hayo ya Chiromo na picha na video zinamuonyesha Omondi akiwa katika hali ya huzuni.

Katika moja ya video, Omondi anaonekana akilia kwa huzuni huku mpenziwe Lynne na mchekeshaji mwenza, Terence Creative wakimakribia na kumshikilia kumpa faraja.

Omondi aliwasili asubuhi ya Ijumaa kutoka nyumbani kwao Sega, Siaya alikoenda wiki jana baada ya kukamilika kwa tamasha la mwisho kumuenzi Fred Omondi katika ukumbi wa Carnivore jijini Nairobi.

Tamasha hilo liliandaliwa na kundi la wachekeshaji humu nchini wakiongozwa na Churchill.

Baadae, mwili wa Fred Omondi utasafirishwa hadi Siaya na mazishi yake kufanyika Jumamosi ya Juni 29, kulingana na ratiba ya mipangilio ya mazishi iliyotolewa wiki jana.

Fred Omondi alifariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni mdogo wake Eric Omondi, na kaka wa pekee aliyekuwa amesalia kwa Eric baada ya kaka yao mwingine kufariki mwaka 2018.

Pole sana Eric!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved