logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kajala: Harmonize alionesha mwanangu uchi wake na bado nikamrudia, siwezi kujisamehe kamwe!

Kwa kumrudia Harmonize licha ya kujaribu kumtongoza bintiye, Kajala alisema kwamba hawezi kujisamehe .

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 June 2024 - 12:54

Muhtasari


  • • “Nikikumbuka hiyo siku, naona kwamba nilijali mapenzi kuliko mtoto wangu na hii kitu siwezi kujisamehe kamwe, siwezi,” alisema.
amejibu madai ya Harmonize.

Mwigizaji Fridah Kajala Masanja ameonekana kujuta kwa hatua yake ya kumrudia msani Harmonize kimapenzi mwaka 2022 baada ya kuachana mwaka 2021.

Katika video ambayo imeibuka upya kutoka kwa kipindi cha uhalisia ambacho yeye na bintiye Paula walikuwa wanazungumzia masuala mbalimbali yanayozunguka maisha yao maarufu kama ‘Behind The Gram’ kupitia runinga ya Zamaradi, klipu hiyo inamuonyesha Kajala alitoa tamko la kujutia hatua hiyo.

Kwa maneno yake, Kajala alisema kwamba sasa hivi ndio anagundua kwamba alifanya makosa makubwa ya kuendekeza mapenzi kwa kumrudia Harmonize licha ya kuwa kilichofanya kuachana naye ni kisa cha yeye [Harmonize] kujaribu kumtongoza bintiye Paula wakati bado walikuwa kwenye mapenzi.

Kwa kumrudia Harmonize licha ya kujaribu kumtongoza bintiye, Kajala alisema kwamba hawezi kujisamehe hata kidogo.

“Nikamrudia mwanamume ambaye aliweza kudiriki kumtupia picha za utupu mwanangu, kwa sababu hata nikikumbuka ile siku ambayo tulikuwa tuko mle ndani, tena nimelala na mwanangu, nakumbuka sikuweza kulala kwa sababu Paula hakuweza kulala, ilibidi nimpakate usiku mzima kwenye mapaja yangu,” Kajala alsimulia kwa uchungu.

“Nikikumbuka hiyo siku, naona kwamba nilijali mapenzi kuliko mtoto wangu na hii kitu siwezi kujisamehe kamwe, siwezi,” alisema.

Hata hivyo, baada ya kumrudia Harmonize na kufanya bonge la Tafrija Mlimani City mnamo Juni 2022, uchumba wao haukukaa sana kwani miezi sita baadae walitengana.

Baadae Paula alikuja kuchumbiana na msanii Marioo na miezi michache iliyopita walibarikiwa na mtoto wa kike pamoja, huku Harmonize naye akijipatia mpenzi mpya kwa jina Poshy Queen.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved