Mwanasosholaiti Zari Hassan ameanza mwezi mpya wa Julai kwa kuzindua mtindo mpya wa nywele fupi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alichapisha rundo la picha zake akionyesha muonekano wake mpya, huu akijivunia mtindo wa nywele fupi.
“Ikiwa inakufurahisha, basi sio kupoteza wakati #shorthairvibes” Zari aliandika kwenye picha hizo.
Mashabiki wake walimsifia kwa muonekano mpya, wengine wakimtaka kudumisha muonekano huo badala ya ule wa mawigi marefu.
Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake;
“Je, unaweza kuweka nywele hii kama milele? 😃 Inaonekana vizuri sana kwako. Kuzeeka nyuma!!!!” Ruth Klenam.
“Ni mrembo kweli, likes za zari jman’ Martha Raphael.
“Nywele inaonekana ya kushangaza kwako.” Galston Anthony.
“Yeye ndiye mwanamke mrembo zaidi nchini Uganda na Afrika Kusini” Rodney Greyssal.
Mama huyo wa watoto watano katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipunguza kuweka wazi kuhusu maisha yake ya mitandaoni.