Mkuza maudhui wa mtandao wa YouTube, Diana Marua alikosa maneno ya kusema baada ya bintiye, Heaven Bahati mweney umri wa miaka 6 kumuonyesha pete yake ya uchumba.
Diana alikuwa amejiandaa kutoka kukutana na baadhi ya mashabiki wake na kusherehekea kupokezwa Kitufe ch Dhahabu kutoka YouTube baada ya kufikisha wafuasi milioni 1 mapema mwezi Februari mwaka huu.
Diana alikutana na bintiye nje na kumuonesha pete zake mbili akimfafanulia bintiye kwamba moja ni ya urembo na nyingine ni ya kuonyesha uhusiano wake wa kimapenzi na mumewe, Bahati Kioko.
Kwa mshangao, Heaven pia alimuonyesha mama yake pete mbili kwenye vidole vyake mkononi na kusema moja ni ya urembo na nyingine ni kwa ajili ya ‘mumewe’, akisema kwamba yuko tayari kuolewa siku wazazi wake watamruhusu kutoka bila kuomba ruhusa.
“Kwa sasa nimeolewa na watu wawili,” Heaven Bahati alisema kabla ya mamake kumkatisha na kumwambia kwamba angependa aje kuolewa na mtu mmoja baadae mbeleni.
“Hata wewe mama naona uko na pete mbili, na mimi hii moja ni ya urembo na nyingine ni ya kuwajibisha penzi kwa mume wangu. Sikuambii mume wangu yuko wapi, ninaenda kumkuta siku nyinyi mtaniruhusu kwenda ninakotaka,” binti huyo alisema.
Akionyesha mshangao wake, Diana alisema kuwa vijana wa kizazi cha Alpha ndio wanakuja kwa kasi Zaidi kuliko wale wa Gen Z kwani kila kitu wanataka sasa kushindana na watu wazima.
“Gen Alpha ndio hawa sasa 🤣🤣🤣🤣 Bora uanze kuwaelewa 😫 Kupigania haki zao za kuolewa wakiwa na miaka 6 bila msamaha 🙆🏽♀️ Sasa huyu @heavenbahati tumsaidie aje???? Je, tuko kwenye ushindani?” Diana alisema.
Tazama video hiyo hapa chini;