logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chipukeezy ajipata pabaya baada ya kukashifu maandamano, kuonyesha kuunga mkono serikali

Kundi la wanamtandao lilimkosoa huku wakimshauri dhidi ya kuzungumza vibaya kuhusu maandamano

image
na SAMUEL MAINA

Burudani03 July 2024 - 10:02

Muhtasari


  • •Chipukeezy alibainisha kuwa rais tayari amewasikiliza vijana wanaoandamana kwa kuondoa Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024.
  • •Kundi la wanamtandao lilimkosoa huku wakimshauri dhidi ya kuzungumza vibaya kuhusu maandamano.
akimsalimia Rais William Ruto.

Mchekeshaji mashuhuri wa Kenya Vincent Mwasia Mutua almaarufu Chipukeezy amejipata pabaya mtandaoni kufuatia kauli yake ya hivi punde kuhusu maandamano yanayoendelea.

Mchekeshaji huyo wa zamani wa Churchill Show mnamo Jumatano asubuhi alitoa maoni yake kuhusu maandamano hayo ambapo alionekana kulaani matukio ya hivi majuzi ambayo yameshuhudiwa katika wiki mbili zilizopita wakati wa maandamano ya kupinga muswada wa fedha na ya kupinga serikali

Chipukeezy alibainisha kuwa rais tayari amewasikiliza vijana wanaoandamana kwa kuondoa Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 ambao ndio chimbuko la maandamano hayo.

"Nchi yetu inaelekea katika mwelekeo hatari, na tunaweza kupoteza mengi ikiwa hatutabadilisha mkondo. Hatuwezi kujenga taifa kwa kulibomoa. Inapingana na kusema tunapigania vijana huku tukidhuru biashara zao na kuhatarisha maisha yao. Vijana walipotoa wasiwasi kuhusu mswada wa fedha, rais aliuondoa. Hii inaonyesha kuwa uchumba wenye kujenga unafanya kazi,” Chipukeezy alisema kupitia Instagram.

Alibainisha kuwa maandamano yamekuja na athari mbaya na kuwataka watu kukumbatia mabadiliko kupitia njia zingine zinazofaa.

"Maandamano yanaunda jukwaa zuri la machafuko na uhuni iwe ya asili au ya kulipwa na inatuongoza kwenye njia mbaya. Niko tayari kutopendwa kusema ukweli wangu. Mabadiliko ya kweli huja kupitia njia sahihi. Iwapo unaona kuwa nchi iko kwenye mkondo mbaya, jihusishe- kwa kugombea wadhifa au kwa kumpigia kura mtu ambaye atawakilisha maoni yako ipasavyo wakati huo ukifika,” alisema.

Maoni hayo aliyoyatoa akiwa safarini Rwanda hata hivyo yalipokelewa kwa mitazamo tofauti huku wengi wakionekana kutokubaliana naye.

Kundi la wanamtandao lilimkosoa huku wakimshauri dhidi ya kuzungumza vibaya kuhusu maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea.

Soma maoni ya baadhi ya wanamtandao;

Sammyro_: I have so much respect for you bro lakini you cannot blame peaceful protestors. Kama karao wangechangamka kulinda duka za watu badala kuharrass watu imagine chaos hazingekuwa. Nakuheshimu bro lakini I beg to differ.

Effykaydesiree: I wish you continued keeping quiet the way you've been quiet all along😢

Carolkariukii: Ukishiba funika tumbo

Willisraburu: Hmmmm…

Abisho_93: Good message wrong pictures 😢

WanjikuStephens: We cannot call peaceful protesters hooligans .You should tell us who paid the goons to disrupt peace.How much money have they paid you? .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved