Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha Auntie Boss, Nyce Wanjeri amewarejesha nyuma mashabiki wake katika kumbukumbu za maisha yake ya utotoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nyce Wanjeri amesimulia mara ya kwanza katika maisha yake alipotaguzana na matumizi ya kopo la msalani au ukipenda karatasi ya tishu.
Wanjeri ambaye mwaka mmoja uliopita alikaribisha mtoto wake wa kwanza na mumewe Leting amewashangaza baadhi ya mashabiki wake kufichua kwamba katika maisha yake ya utotoni hakuwahi kutumia karatasi ya tissue katika shughuli za usafi wa chooni hadi pale alipoingia kidato cha kwanza.
Hii ina maana kwamba maisha yake ya masomo ya shule ya msingi, Wanjeri alitumia tu mbinu nyingine za kujihakikishia usafi baada ya shughuli za chooni.
“Ulianza kutumia tissue paper ukiwa how old ? Mimi from form one,” alisema.
Wanjeri alisema kwamba kuingia shule ya upili kumfungulia fursa adimu ya kutumia karatasi ya tishu, kwani matumizi ya tishu yalikuwa yanaonekana kama ni ustaarabu wa watu wenye navyo.
Alisema kwamba walikuwa wanalazimika kutumia majani ya miti na wakati mwingine magazeti ambayo babu yake alikuwa anapata kutoka kwa mhudumu wa duka la hoteli karibu na nyumbani kwao.
“Before ilikuwa majani Na gazette guka alikuwa anabook Kwa kahoteli Fulani,” aliibua kumbukumbu.
Ungamo hili lilivutia maoni kutoka kwa baadhi ambao walikumbuka kutumia mbinu mbadala kama hizo kuhakikisha usafi baada ya shughuli za chooni.
“Kwanza hyo Majani ilikua inamea karibu na choo.. Sijui ni ju ya "fertilizer"” @melissakaboi.
“Ya kwanza ilikua ile ya blue 😂. At around 10 years old wajameni “ @wanjikuwanjiku.
“Vitu Kam tissue nimejua Kama Niko college BT huwa natumia Tu nikiwa shule BT nikifika shamakhokho yaan homeland tunatumia tissue ingne original inaitwa KAMANG,ULIA only luhyas understand,” @kibindutiktoker
Kumbukumbu zako kuhusu mara ya kwanza kutumia karatasi ya tishu ni zipi na ilikuwa lini?