Akothee ammiminia mahaba mpenzi wake Nelly Oaks, azungumzia uhusiano wao wa kipekee

Pia alikiri kuhusu kusababisha drama kidogo wakati mwingine ili tu kunasa umakini wa mpenzi wake.

Muhtasari

•Meneja rasmi na mpenzi wa mwimbaji maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu  Akothee, Nelly Oaks anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

•“Ndiyo, nina makosa yangu, lakini jinsi unavyokubali, kunikumbatia na kunipenda ni ushuhuda wa moyo wako safi," Akothee alisema.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Bw Hezekiah Nelson Oyugi almaarufu Nelly Oaks, meneja rasmi na mpenzi wa mwimbaji maarufu wa Kenya Esther Akoth (Akothee), anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Akothee ametumia siku hii maalum kumthamini mwanamume huyo ambaye ana nafasi muhimu sana maishani mwake na kusherehekea uhusiano wao wa kimapenzi.

“Leo, katika siku hii ya pekee, ningependa kutoa shukrani zangu nyingi kwa wazazi wako kwa kuupa ulimwengu vito hivi vyenye thamani. Babe, maneno hayana uwezo wa kukamata kina cha uthamini wangu na upendo wangu kwako. Safari yetu pamoja, iliyo na heka heka nyingi, inadhihirisha tu nguvu ya uhusiano wetu,” Akothee alimwandikia Nelly Oaks kupitia Instagram.

Mama huyo wa watoto watano aliendelea kufunguka jinsi wanavyotofautiana nyakati fulani katika mahusiano yao hadi kufikia hatua ya yeye kutishia kuondoka, lakini hatimaye wanatatua masuala yao pamoja na kuendelea kufurahia uhusiano wao.

Pia alikiri kuhusu kusababisha drama kidogo wakati mwingine ili tu kunasa umakini wa mpenzi wake.

"Wewe ni rafiki yangu mkubwa, mwamba wangu, na nuru inayoangaza moyo wangu. Unajua kuwa wewe ndiye pekee kwangu. Katika siku hii maalum, kumbuka jinsi ulivyo muhimu si kwangu tu, bali kwa Wakenya wote. Vita ambavyo umepigania kwa ajili yangu, kujitolea ulikojitolea, na changamoto ambazo tumekabiliana nazo zimeimarisha uhusiano wetu tu,” aliambia Nelly Oaks.

Aliongeza, “Ninatabasamu hadi kwenye benki na Brand Akothee kwa sababu yako. Wakati wowote kampuni inalipa, au mkataba mpya ukishuka wewe ndiye mtu wa kwanza ninayekupigia simu, ninakupigia simu ili kushiriki furaha yangu na kukufanya ujivunie.”

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alimaliza kwa kukiri kumpenda sana Nelly Oaks na pia akathamini upendo ambao mwanamume huyo maalum maishani mwake anamuonyesha.

“Ndiyo, nina makosa yangu, lakini jinsi unavyokubali, kunikumbatia na kunipenda ni ushuhuda wa moyo wako safi. Nakupenda sana, Dkt Hezekiah Nelson Oyugi. Heri ya kuzaliwa, mpenzi wangu!,” aliandika.

Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa muda mrefu sasa. Hapo awali waliwahi kuachana, huku Akothee hata akichukua hatua ya kuolewa na mwanamume mwingine, lakini hatimaye walirudiana na kuendelea na uhusiano wao.