Mchungaji mmoja amezua minong’ono mingi katika mtandao wa kijamii baada ya kuonekana akiwahubiria waumini katika kanisa lake akitabiri kwamba atakuwa kama Yesu katika kipindi cha miaka 500 ijayo.
Video hiyo yenye utata ya mchungaji wa Ghana aliyetambulika kwa jina Stephen Adom Kyei-Duah, alionekana bila hiana akidai kwamba atachukua nafasi ya Yesu Kristo katika maisha ya wanadamu katika miaka 500 ijayo.
Katika mahubiri hayo, mchungaji huyo alionekana akiwaambia waumini wake kwa sauti ya kutisha kwamba picha zake zitakuwa zinasambazwa kwa Wakristu kote duniani na wataziweka kwenye kuta za nyumba zao wakimuangalia na kumtafsiri kama Yesu.
Katika video hiyo, Mchungaji Kyei-Duah anatangaza kwa ujasiri kwa waumini wake kwamba picha zake zitachukua nafasi ya zile za Yesu Kristo katika kipindi cha karne tano zijazo.
Mchungaji Kyei-Duah alitangaza wakati wa mahubiri, “Picha zangu zitachukua nafasi ya Kristo katika miaka 500 ijayo.”
Kauli ya mchungaji huyo imezua dhoruba ya ukosoaji na kutoamini mtandaoni, huku watumiaji wengi wakionyesha kushtushwa na kutokubali madai hayo ya kufuru.
Tazama video hiyo hapa kisha utoe maoni;