logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vanessa Mdee aeleza safari yake na tatizo la jicho

Licha ya kutafuta ushauri wa madaktari kadhaa,hakuna aliyebainisha kiini cha Vanessa kuwa na shida ya retina

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 July 2024 - 13:51

Muhtasari


  • •"Nilitua Nairobi Jumapili na kulala. Ilipowadia Jumatatu asubuhi, niliamka na maumivu makali kwenye jicho langu la kushoto kwani sikuweza kuelewa ilikuwa nini." Alinena Vanessa
  • •Licha ya kutafuta ushauri wa madaktari kadhaa, hakuna aliyeweza kuonekana kubainisha kiini cha mama huyo mwenye watoto 2 kuwa na shida ya kizuizi cha retina 

Mwanamuziki wa Tanzania, Vanessa Mdee hatimaye amefungua roho kuhusu jinsi alivyokumbana na matatizo ya macho.

Pia, alielezea safari yake ya upasuaji wa kurekebisha hali hiyo na hofu aliyokuwa nayo wakati wa kipindi hicho.

Kupitia chaneli yake ya YouTube inayoitwa Vee na Roo, mama wa watoto 2, alisimulia mwanzo wa safari yake ya ulemavu wa macho huku akisimulia:

“Mwaka 2015 nilienda Nairobi, Kenya kwenye Coke Studio na Burna Boy tukawa tunatumbuiza, ilikuwa ni furaha sana.

Nilitua Nairobi Jumapili na kulala. Ilipowadia Jumatatu asubuhi, niliamka na maumivu makali kwenye jicho langu la kushoto kwani sikuweza kuelewa ilikuwa nini.

Niliieleza timu yangu ila sikutaka kufanya jambo kubwa kutokana na hali hiyo."

Alieleza jinsi ambavyo, kinyume na matarajio yake, maumivu hayakuisha bali yalidumu kwa wiki nzima jambo ambalo lilimlazimu kutafuta msaada wa matibabu.

"Maumivu yalizidi kuwa mabaya kadri wiki ilivyokuwa inasonga. Nilienda kuonana na mtaalamu ambaye alisema kuwa nilikuwa na shida ya retina.

Sikuelewa hapo nyuma, lakini baada ya muda nimezidi kuwa na taarifa zaidi.

Nilikuwa nikipoteza uwezo wa kuona siku baada ya nyingine...

Niliingia kwenye utaratibu fulani wa dharura na daktari akajitahidi kadiri alivyoweza bila mafanikio.

Kwa hivyo niliishia kupoteza macho yangu takriban siku 10 baadaye. Kwa mtu aliyezaliwa na macho mawili ya kuona, ilikuwa pigo kubwa," mtayarishaji wa maudhui alisema.

Vanessa ambaye sasa anaishi Marekani, alieleza kwa uwazi alipokuwa akiwatembeza mashabiki wake kwenye kumbukumbu na historia ya kisa chake.

Licha ya kutafuta ushauri wa madaktari kadhaa, hakuna aliyeweza kuonekana kubainisha kiini cha mama huyo mwenye watoto 2 kuwa na shida ya kizuizi cha retina.

Vanessa, alipata changamoto mpya huku akikumbana na masaibu kama ugumu wa kuendesha gari kati ya mambo mengine machache.

Hali hii imlazimisha kuchukua mapumziko kutoka kwa mitandao ya kijamii.

"Namshukuru Mungu kwa upasuaji wa kurekebisha na sayansi iliyotumika.

Nilifanyiwa upasuaji wa misuli ya macho ambao uliniwezesha mboni za macho kurejea mahali pake...upasuaji ulifanikiwa sana na namshukuru Mungu.

Macho yangu bado hayajarudi  kwa asilimia mia moja, lakini kwa hakika tutafika huko."Alimalizia msanii huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved