logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Drake apoteza bet ya Ksh 38M baada ya Argentina kuichabanga Kanada kwenye nusu fainali

Kanada ilibanduliwa kwenye nusu fainali na Argentina kwa kipigo cha mabao 2-1

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 July 2024 - 05:49

Muhtasari


  • • Drake aliwekeza kitita cha dola elfu 300, sawa na shilingi milioni 38.29 pesa za Kenya akitumai Kanada wangeipiga Argentina yake Messi kwenye nusu fainali hiyo.
DRAKE

Msanii kutoka Kanada, Drake si mgeni katika suala la kucheza Kamari katika michezo mbalimbali, iwe ndondi, tenisi na hata kandanda.

Katika michuano inayoendelea ya Copa America, Drake alitupa ndoana yake kwenye Kamari akijaribu bahati kwa kuibashiria timu yake ya nyumbani, Kanada kuwashinda mabingwa watetezi Argentina kwenye nusu fainali.

Drake aliwekeza kitita cha dola elfu 300, sawa na shilingi milioni 38.29 pesa za Kenya akitumai Kanada wangeipiga Argentina yake Messi kwenye nusu fainali hiyo.

Hata hivyo, matokeo yalikuwa kinyume chake kwani Kanada ilibanduliwa kwenye nusu fainali na Argentina kwa kipigo cha mabao 2-1

Rapa huyo angeshinda kitita cha dola milioni 2.88, sawa na shilingi za Kenya milioni 368 ikiwa Canada ingefanikiwa kuipiga Argentina.

Chapisho la Drake kuhusu dau hilo ni pamoja na nukuu iliyosema, "Hili linaweza kumpata Messi" akiwa na emoji ya bendera ya Kanada.

Mbio za Canada hadi nusu fainali zilikuwa mshangao mzuri katika mashindano hayo. Kikosi cha kocha mkuu Jesse Marsch kiliingia Copa América nafasi ya 11 kati ya timu 16 kulingana na viwango vya FIFA.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kanada kuonekana kwenye Copa America. Timu ya taifa ya wanaume ilikuwa inatafuta taji lake la kwanza katika mchuano mkubwa tangu Kombe la Mataifa ya Amerika Kaskazini mnamo 1990.

Mechi ya Jumanne ilikuwa ni mechi ya pili ya ana kwa ana na Argentina katika Copa America. Canada ilipoteza 2-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi la timu zote mbili mnamo Juni 20.

Huo ulikuwa mkutano wa pili kuwahi kati ya nchi hizo mbili. Ya kwanza ilikuwa mechi ya kirafiki ya 2010 ambayo Argentina ilishinda 5-0.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved