logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vera sidika adai wanaume Gen Z wamefurika DM baada ya kusema ni mafundi kwenye mapenzi

“Nasikia Gen Z wanajua kuchapa hiyo kitu, ni kweli ama uongo? ' Sidika alikuwa ameuliza.

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 July 2024 - 10:47

Muhtasari


  • • Hata hivyo, mmoja alimpa suluhu kwamba afanye mkutano wa ana kwa ana na wao na kuchagua mmoja ambaye jicho lake litavutiwa naye.
VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti Vera Sidika ameibua madai kwamba DM zake zimefurika na jumbe kutoka kwa vijana wa kiume wa Gen Z ambao wengi wao wanamuomba fursa ya penzi lake.

Hii ni baada ya Sidika kuandika kwa utani kwenye insta story yake akizungumzia tetesi za wanaume wa Gen Z kuwa mafundi hodari katika suala la mapenzi na kumalizia kwa ithibati kwamba yuko single.

“Nasikia Gen Z wanajua kuchapa hiyo kitu, ni kweli ama uongo? Na kusema ukweli mimi niko single,” Vera Sidika aliandika kwenye insta story hiyo ambayo sasa imefutika baada ya kumaliza saa 24.

Katika sasisho jingine saa kadhaa baadae, Sidika alirudi kwenye instastory yake na kusema kwa mshangao kwamba haamini macho yake maelfu ya jumbe kutoka kwa wanaume wa Gen Z kwenye DM yake ambao walikuwa wanamuomba nafasi ya kumhamisha kutoka kwenye kategoria ya kuwa single.

Hata hivyo, Sidika alisema kwamba kibarua kigumu ambacho atakuwa nacho ni kuchagua anayestahiki nafasi ya kumpenda kutoka kwa wanaume zaidi ya elfu moja wa Gen Z kwenye DM yake.

“Bado niko kwenye mshangao. DM yangu iemgeuka kuwa wazima, kusema kweli. Ni vipi mtu anaweza kumchagua mmoja kati za maelfu ya Gen Z kwenye DM, wueeh. Nimeganda kaitka kipindi cha siku mbili zimepita, ndio naendelea kupata nafuu,” Vera Sidika alisema.

Hata hivyo, mmoja alimpa suluhu kwamba afanye mkutano wa ana kwa ana na wao na kuchagua mmoja ambaye jicho lake litavutiwa naye.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved