logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Amber Ray: “Nitafeli kama mama ikiwa mwanangu atafikira mimi ni muhimu kuliko mkewe”

“Ninamlea mwanangu kuwa mwanaume, baba na mume. Siji mbele ya familia yake ya baadaye,” aliongeza.

image
na Davis Ojiambo

Burudani11 July 2024 - 06:02

Muhtasari


  • • “Jambo moja ninalojua ni kwamba, Iwapo mwanangu atakua na kufikiria kuwa ninakuja mbele ya mke wake, basi nimeshindwa kama mama,” Ray alisema.

Amber Ray ni mmoja kati ya kina mama wachache ambao wana mrengo wa kimawazo kwamba mtoto anapooa, anastahili kumweka mkewe mbele kwa kila kitu kalba ya wazazi wake.

Mama huyo wa watoto wawili aliweka mawazo haya bayana kupitia ukurasa wake wa Instagram alipochapisha picha ya pamoja na mwanawe wa kwanza, tineja Gavin.

Ray alisema kwamba mama yeyote anafaa kujua kwamba amefeli katika majukumu yake ikiwa mwanawe ataoa na bado awe anamuona mzazi wake kuwa wa maana kabla ya mkewe na wanawe.

“Jambo moja ninalojua ni kwamba, Iwapo mwanangu atakua na kufikiria kuwa ninakuja mbele ya mke wake, basi nimeshindwa kama mama,” Ray alisema.

Mkewe Kennedy Rapudo aliradidi kwamba kila mama, sawa na yeye wanastahili kujua kwamba wanapowalea wanao wa kiume, jukumu ni kuwafunza jinsi ya kuwajibikia familia zao wenyewe na wala si kuwathamini wazazi zaidi kuliko mke na watoto wao.

“Ninamlea mwanangu kuwa mwanaume, baba na mume. Siji mbele ya familia yake ya baadaye,” aliongeza.

Baadhi ya mashabiki wake walikubaliana naye, wengine wakisema kwamba wanaazimia kuwakuza wanao wa kiume jinsi ya kuwathamini wanawake kwenye jamii, kinyume na vizazi vilivyopita ambavyo wanawake walichukuliwa kama pambo tu kwenye jamii.

“Siku zote nitamwambia mwanangu msichana akipata mimba kamwe usimtupe wala kuinua mikono juu ya wanawake ni makosa!!!!tuwalee waungwana sio wavulana tena.” @dark_girl_katie

“Hili ndilo lengo langu kama mama single. Anapaswa kumtendea kila mtu kwa heshima haswa mke wake” @tixxie254.

“Hatusikii hili sana 👏👏, ukweli kwamba unamlea kuwa mwanafamilia basi,,,, wewe ni icon kwa kweli” mwingine alisema.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved