Mwimbaji na mtunzi maarufu wa nyimbo kutoka Nigeria Davido aliibua hisia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka uadui pembeni na kumtumia ujumbe maridhawa Wizkid wakati alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 34.
Hii ilifunuliwa katika video mpya inayofanya misele kwenye jukwaa maarufu la media ya kijamii TikTok.
Katika video hiyo, Davido alisikika akiimba wimbo huo wa furaha ya kuzaliwa akiwa ndani ya ndege binafsi huku akisindikizwa na rafiki yake mmoja ambaye pia aliimba pamoja na kumshangilia staa huyo, Wizkid.
Akimpa maua yake, Davido alimtaja Wizkid kama gwiji wa muziki kuwahi kutokea katika tasnia ya muziki wa Afrobeats.
Akiimba kusherehekea nyota huyo, Davido aliimba: ‘Happy birthday to you, shout-out to my niggah Wiz, I love you. Wewe ni ljendari.’
Matakwa ya Davido kwa Wizkid kwenye siku yake ya kuzaliwa yalivutia hisia za watu wengi ambao walivamia ukurasa wa maoni wa chapisho hilo ili kutoa mawazo yao.
Baadhi walihisi kitendo cha Davido kumsherehekea adui wake nambari moja ni ukomavu wa hali ya juu ambao unafaa kuigwa na wasanii wengine.
Itakumbukwa kwa miaka mingi, Davido na Wizkid wamekuwa wakihasimiana huku wakichokozana kwa maneno makali mitandaoni.
Ya hivi punde, Wizkid alimtupia Davido matusi makali ambayo yalisababisha mashabiki wao kupapurana kwenye mitandao ya kijamii, kila mmoja akivuta upande wa msanii anayemuunga mkono.