logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Donna azungumzia changamoto za kuwa single mother siku chache baada ya kupata mtoto

“Mimi nafikiri uzazi unaweza kuwa changamoto lakini ni changamoto nzuri zaidi mtu anaweza kuwa nayo."

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 July 2024 - 08:19

Muhtasari


  • • “Mimi nafikiri uzazi unaweza kuwa changamoto lakini ni changamoto nzuri zaidi mtu anaweza kuwa nayo." alisema.
TANASHA DONNA.

Mwanamitindo na msanii Tanasha Donna amezungumzia jinsi alianza kuyatazama maisha upya kwa lenzi tofauti baada ya kuwa mama kwa mara ya kwanza katika maisha yake.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Rwanda kama moja ya mkakati wa kuandaa ujio wa albamu yake wiki kesho, Donna alisema kwamba japo kuwa mama ndicho kitu cha kujivunia zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake, kulikuwa na changamoto si haba.

Msanii huyo ambaye ni mpenzi wa zamani na mzazi mwenza na Diamond Platnumz, alisema kwamba alipitia msururu wa changamoto ikizingatiwa kwamba ndio ilikuwa mara ya kwanza kuwa mama, na ghafla akajipata nje ya ndoa na mtoto mchanga.

“Mimi nafikiri uzazi unaweza kuwa changamoto lakini ni changamoto nzuri zaidi mtu anaweza kuwa nayo. Uzazi ndicho kitu kizuri zaidi ambacho kiliwahi kutokea kwangu, ilibadilisha maisha yangu, na kuifanya iwe kwamba si kila kitu ni kuhusu mimi bali sasa nilikuwa na kusudi, nilichokuwa nafanya sasa ni kuhusu mtu mwingine sasa – Naseeb Jr,” Donna alisema.

Akizungumzia baadhi ya changamoto hizo, Tanasha Donna alisema;

“Changamoto zinaweza kuwa kwa mfano wakati ndio mara yako ya kwanza kuwa mama, unatoka katika ndoa yako, kumaanisha kwamba ndio mara ya kwanza pia kuwa single mother [lakini kwa sapoti ya babake], ila ninapozungumzia kuhusu kuwa single mother namaanisha muda mwingi ni mimi ninaishi naye (Naseeb Jr) hata kama anamtembelea babake mara kwa mara, lakini nafikiri changamoto kuu ni kuwa mama kwa mara ya kwanza kwa sababu hakuna kitabu cha kutoa mafunzo ya jinsi ya kuwa mama, unajua, huwezi kuwa mama mkamilifu, unajifunza kadri muda unavyozidi kusonga.”

Ndoa ya Donna na Diamond ilisambaratika mwaka 2020, miezi michache baada ya kukaribisha mwanao, Naseeb Jr ambaye anatajwa kushabihiana moja kwa moja na babake kwa sura.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved