Mtayarishaji wa maudhui Thee Pluto ametoa neno la ushauri kwa wanaume wote kuhusu maisha.
Akizungumza kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram, aliwapea wanaume ushauri kwamba watafute pesa kwanza kabla ya kufikiria wanawake.
Thee pluto amewataka wanaume wote kuhakikisha vipaumbele vyao vinakuwa vya kwanza kwenye mambo ya maana kuliko kuzingatia mambo ambayo yanaweza kuja baadaye.
Thee Pluto alisema kuwa kutafuta pesa kwanza kabla ya kuanza kufikira kuanza Maisha na mwanawake ni vizuri.
Kwani wanawake hawa watahitaji pesa kufanya mambo kadhaa, mtu atahitaji kumlisha, na hautamlisha kwa maneno matamu tu ya mapenzi. Utahitaji pesa katika kesi hii.
"Usipendane na mwanamke kabla ya kupenda pesa." Pluto aliandika.
Pia alieleza kuwa, mwanaume ni vyema ukaweka ndoto zako mbele ya wanawake kwani kwa njia hiyo unaweza kushinda tu badala ya kutaka kufanya kinyume.
"Mwanaume anayetoa ndoto zake kwa mwanamke huishia kupoteza zote mbili!!" Pluto aliandika, akimjibu shabiki wake.
Thee Pluto ni miongoni mwa wafanyabiashara wachanga zaidi wa biasharaForex.