logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mrembo,39, bila mume awacheka wanarika wenza walionyenyekezwa na maisha baada ya kuolewa

Akiashiria ukosoaji wao wa hapo awali, Toke Makinwa alionyesha uamuzi wake wa kupanua neema sawa kwao.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 July 2024 - 10:15

Muhtasari


  • • Makinwa alisema kwamba wengi wao licha ya kuwa katika ndoa, bado wanachepuka ili kupata hela za matunzo kwani ndoa imewanyenyekeza kimaisha.
TOKE MAKINWA

Vlogger na mjasiriamali wa Nigeria, Toke Makinwa anawakejeli wanawake walioolewa, hasa watu mashuhuri ambao alidai kwa muda mrefu walikuwa wanamsengenya kwa hali yake ya kutoolewa licha ya kuwa na umri mkubwa.

Makinwa ambaye ana umri wa miaka 39 bila mume wala mtoto alipeleka kwenye ukurasa wa Instagram na kuweka ujumbe wa kuwakebehi wanarika wenza walioolewa na ambao alidai wanateseka katika ndoa.

Makinwa alisema kwamba wengi wao licha ya kuwa katika ndoa, bado wanachepuka ili kupata hela za matunzo kwani ndoa imewanyenyekeza kimaisha.

Mtangazaji huyo wa BBNaija aliwaita wanawake ambao hawakutajwa ambao wanajionyesha kuwa wameolewa lakini wanabaki kupatikana kwa wanaume wengine.

Akiashiria ukosoaji wao wa hapo awali, Toke Makinwa alionyesha uamuzi wake wa kupanua neema sawa kwao.

“S/O watu wote waliokuwa wakinihukumu. Sasa kwa kuwa maisha yamekutembelea, nitakuonyesha neema. Mwanamke umeolewa lakini bado uko sokoni. Hii ndiyo sababu sikuwahi kumhukumu mtu yeyote. Tazama jinsi maisha yamekufedhehesha sasa, Love you still,” aliandika.

Katika chapisho lingine, alichukua U-turn huku akituma mapenzi na mwanga kwa wanawake walioolewa ambao wana hatia ya kauli yake.

“Tusitikise meza. Upendo na mwanga," alisema.

Mwanamitndo huyo mwenye utata aliwahi kiri kwamba anajuta pakubwa kujichubua.

Aliandika, "Hakuna. Majuto yanachosha sana!!!! Subiri, labda kuchubua ngozi yangu, lilikuwa jambo la kipumbavu zaidi na ninashukuru sana kwa jeni nzuri na pesa, vinginevyo…”

Alikuwa anamjibu mtumizi mmoja wa X aliyetaka kujua kama kuna kitu au jambo ambalo aliwahi kulifanya na kuja kulijutia ukubwani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved