Mtangazaji wa Radio Jambo, Gidi Ogidi amemtetea vikali mwanaridha wa Kenya katika mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala baada ya kumaliza wa mwisho katika nusu fainali ya Olimpiki mjini Paris, Ufaransa.
Omanyala alishindwa kutinga kwenye fainali ya mbio hizo na kutemwa nje baada ya kumaliza katika nafasi ya mwisho kwenye nusu fainali.
Kutokana na matokeo hayo, Wakenya walionyesha kutoridhishwa kwake na ukimbiaji wa mwanamume huyo aliyetajwa kuwa mwenye mbio zaidi barani Afrika.
Hata hivyo, mtangazaji huyo wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi alimtetea akisema kwamba anastahili kongole licha ya kushika mkia kwenye nusu fainali.
Kulingana na Gidi, si rahisi kwa mtu kushinda mbio za mita 100 kwani hata taifa la Marekani licha ya kuwa na watimkaji mbio hodari katika 100m kwa miaka mingi, wamekuja kushinda dhahabu ya Olimpiki baada ya miaka 20.
“Tulikuwa na matumaini kwa Kijana wetu Omanyala lakini hadi utambue Marekani yenye wanariadha wa juu kabisa imeshinda dhahabu hiyo baada ya miaka 20 na ni katika kuamuliwa na picha. Mpe Omanyala mapumziko. Sio rahisi,” Gidi alisema.
Noah Lyles wa Marekani alifikisha ipasavyo wakati ilikuwa muhimu zaidi kwa kushinda fainali yeye ukaribu zaidi kuwahi kutokea ya Olimpiki ya mita 100 kwa elfu tano ya sekunde siku ya Jumapili na kuipa Marekani taji hilo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
Kwa kumalizia blanketi Lyles aliamini kuwa alikuwa amechelewa sana kumnasa Kishane Thompson, lakini skrini kubwa ilimthibitisha kama mshindi katika sekunde 9.79, sawa na Mjamaika, lakini mbele kwa upana wa fulana.