Director Trevor na mpenzi wakec mpya Kikilove Yvonne wanasherehekea miezi 7 tangu walipoanza safari yao ya mapenzi.
Kupitia kurasa zao za Instagram, wapendanao hao walichapisha msururu wa picha za mahaba na kufichua kwamba imekuwa miezi 7 pamoja.
Kikilove Yvonne alifichua kwamba haamini kipindi hiki cha miezi 7 kimepita kwa haraka utadhani ni juzi tu.
“Siwezi Amini Tayari Ni Miezi 7 Tangu Nikutane Na Mtu Huyu Ajabu ❤️ Inahisi Kama Tumekutana Hivi Punde Jana, Hapa Ni Kwa Dakika Nyingi Zaidi Na Kumbukumbu Pamoja Upendo @director_trevor 🌹❤️” Yvonne aliandika.
Itakumbukwa mwezi Februari, Trevor alitangaza rasmi kumaliza uhusiano wake wa miaka 6 na aliyekuwa mpenzi wake na mfanyikazi mwenza katika utengenezaji wa maudhui, Mungai Eve.
Trevor akitangaza wakati huo, aliweka wazi kwamba amempiga kalamu Mungai Eve kutoka kujihusisha na shughuli zozote kwenye akaunti ya YouTube na Facebook, huku akimuachia tu ile yake ya Instagram.
Trevor alipiga hatua zaidi na kubadilisha chapa hiyo kutoka Mungai Eve Media hadi Kenya Online Media na kutangaza kuwaajiri watu wengine kufanya kazi ambayo Mungai Eve alikuwa anajukumika nayo.