logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Furaha ya Karen Nyamu baada ya Edwin Sifuna kusifia muonekano wake mpya na wigi

Seneta wangu wa Nairobi anajaribu kutumia maneno mengi ninaonekana wa moto kwenye wigi langu - Nyamu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 August 2024 - 11:07

Muhtasari


  • Seneta wangu wa Nairobi anajaribu kutumia maneno mengi ninaonekana wa moto kwenye wigi langu - Nyamu.
Karen Nyamu na wigi jipya

Seneta maalum Karen Nyamu hakuweza kuficha furaha yake baada ya mwenzake katika bunge la seneti Edwin Sifuna kusifia muonekano wake mpya.

Nyamu ambaye aliinuka kuchangia hoja yake katika mjadala wa madeni ya kaunti, alikuwa na muonekano tofauti. 

Seneta huyo alibadilisha muonekano wa nywele zake kwa kuja na wigi jipya kabisa ambalo Sifuna alilisifia kuwa ni la dhahabu.

Nyamu alipeleka klipu hiyo ya Sifuna kwenye instastory yake na kuonesha furaha kiranja wa walio wachache kwenye seneti kumsifia.

"Kama ambavyo dadangu seneta Karen Nyamu amesema, ni sharti nikiri kwamba nilikuwa nusra nisimtambue kutokana na taji lake jipya la dhahabu, sikumbuki mara ya mwisho nilimuona akiwa na muonekano huu, lakini iko sawa," Sifuna alisema.

Nyamu kwa upande wake, alisema kwa utani kwamba Sifuna ambaye ni seneta wa jimbo la Nairobi alikuwa anajaribu kutumia lugha changamano kupitisha kauli kwamba alikuwa na muonekano wa moto.

 

"Seneta wangu wa Nairobi anajaribu kutumia maneno mengi ninaonekana wa moto kwenye wigi langu, ah sasa 'iko sawa' ndio nini?" Nyamu alitania.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved