Msanii Harmonize kwa mara ya kwanza amefichua sababu inayomfanya kujitoa kwa njia kubwa kwa kila mwanamke anayeingia katika mapenzi naye.
Akizungumza wikendi iliyopita baada ya tamasha la timu ya Yanga, Harmonize alifichua kwamba yeye Ana mazoea ya kuwafanya wanawake wake kujihusi gahari kuwa katika uhusiano naye.
Boso huyo wa lebo ya Konde Music Worldwide alisema kwamba yeye kuwapa wanawake zawadi za Range Rover na pesa nyingi si kuhonga mapenzi bali ni kujaribu kuwa mkweli.
Alisema kwamba pindi anapoingia katika mapenzi na mwanamke, moja kwa moja wao huwa kitu kimoja na hivyo ku'share mapato yake ni jambo la kawaida.
"Mimi niko tu muwazi na mkweli unajua kwangu mimi mwanamke wangu ni nusu ya sehemu yangu. Nikiwa napambana huwa sipambani peke yangu, nikiwa navuka viunzi sisemi kwamba nataka nifike pale bali nasema nataka tufike pale."
"Hivyo ninavyokuwa na mtu ni sawa na kwamba nabeba msalaba wake kama wa kwangu. Ni kama napambana kwa ajili ya watu wawili na chochote huwa napata najua kwamba kuna mtu amenipa motisha wa kukipata, hivyo nampenda mrembo wangu na ni jukumu langu kuhakikisha Ana furaha, " Konde Boy alieleza.
Harmonize si mgeni katika suala la kuwapa wapenzi wale zawadi kubwa za kutamanisha.
Mwaka 2022, msanii huyo alijitoa kwa mapana na marefu kumfurahisha aliyekuwa mpenzi wake, Frida Kajala kwa kumnunulia gari aina ya Range Rover.
Hata hivyo, uhusiano wao haukuzidi miezi 6 kabla ya kuachana na hakuweza kurudishiwa gari hilo la kifahari.
Harmonize alifunguka haya ikiwa ni siku chache baada ya kuzua uvumi wa kuachana baada ya kufuta picha zao wote na kuacha kufuatiana kwenye mitandao.