logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kutana na mchungaji anayetengeneza zaidi ya Ksh 565K kila siku kutoka YouTube

Mchungaji huyo hupakia takribani video 1,500 kila wiki.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 August 2024 - 10:22

Muhtasari


  • • Juhudi kubwa za mchungaji zinajumuisha takriban video 1,500 kila wiki, kufanya hadhira yake kushughulikiwa na kituo chake kustawi.
Pasta Jerry Uchechukwu Eze

Mchungaji wa kanisa moja nchini Nigeria amegonga vichwa vya habari baada ya taarifa kuhusu mapato anayojizolea kutoka YouTube kuenezwa.

Kwa mujibu wa taarifa, mchungaji Jerry Uchechukwu Eze wa kanisa la Joy International  ndiye anayeongoza nchini humo kwa watu wanaolipwa hela ndefu na jukwaa la YouTube.

 Pasta Eze anasemekana kuwekeza katika video nzuri jambo ambalo linavutia wengi kwa video za mafunzo yake kwenye jukwaa hilo.

Playboard, jukwaa la kuonyesha deta za malipo ya YouTube ilidhihirisha kwamba pasta huyo anatengeneza zaidi ya Naira milioni 7 kila siku kutoka YouTube, kiasi sawa na Ksh 565, 840.

Deta hiyo ilionyesha kwamba mchungaji huyo ndiye anashikilia nafasi ya kwanza kwa wanaolipwa na YouTube nchini humo kwa kupokezwa kiasi cha Naira bilioni 7, sawa na shilingi milioni 564.745 pesa za Kenya.

Deta zilionyesha kwamba mnamo Julai 16, 2023, alipata mapato ya ajabu ya N21 milioni, sawa na shilingi za Kenya 1.7M kwa siku moja kutokana na kuongezeka kwa trafiki ya wageni kwenye ufuatiliaji wa video zake YouTube. 

Chaneli ya kanisa lake ina wafuasi 2.1M wanaofuatilia na maidhui yake aghalabu huwa kutiririsha mikutano ya ibada na maombi. 

Juhudi kubwa za mchungaji zinajumuisha takriban video 1,500 kila wiki, kufanya hadhira yake kushughulikiwa na kituo chake kustawi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved