logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Mwanaume anayekupenda atakudanganya kila wakati kwa sababu anajali hisia zako” - Samidoh

Samidho anaeleza kwamba ishara moja ya mwanamume anayekupenda ni kukudanganya.

image
na Davis Ojiambo

Burudani16 August 2024 - 04:57

Muhtasari


  • • Msanii huyo amekuwa katika mwanga wa lensi za waandishi wa habari za burudani katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mizozo isiyoisha katika maisha yake ya kimapenzi.
SAMIDOH,

Msanii wa Mugithi na afisa wa polisi Samidoh amezua dhana isiyo maarufu kuhusu hulka ya wanaume kuwa wadanganyifu katika mapenzi.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Samidoh alichapisha kauli iliyoonekana kutetea tabia ya wanaume kuwadanganya wanawake wanaowapenda.

Akionekana kuwatetea wanaume na wakati uo huo kuwashauri wanawake katika mduara wa mapenzi, Samidoh alisema kuwa ni kawaida kwa mwanamume kumdanganya mwanamke anayempenda.

Kwa mujibu wa baba huyo wa watoto 5, hali ya mwanamume kuwa na mazoea ya kusema uongo kwa mwanamke anayempenda ni mbinu moja ya kuhakikisha kwamba analinda na kujali hisia za mhusika.

“Mwanaume anayekupenda atakudanganya kila wakati kwa sababu anajali hisia zako. Angependelea kukudanganya kuliko kuumiza hisia zako,” Samidoh alisema.

Msanii huyo amekuwa katika mwanga wa lensi za waandishi wa habari za burudani katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mizozo isiyoisha katika maisha yake ya kimapenzi.

Zogo lilianza mwaka 2021 alipokiri hadharani kwa kuchapisha ujumbe wa kuomba radhi kwa mkewe Edday Nderitu kwa kukiri kuchepuka na ‘kwa bahati mbaya’ kupata mtoto na Karen Nyamu.

Hata hivyo, miezi kadhaa baadae tena alijipata amerudi katika ubavu wa Karen Nyamu na kupata mtoto wa pili, jambo lililomuudhi Edday Nderitu kupelekea yeye kutangaza kujiondoa katika ndoa yake ya miaka 15 kwa kile alieleza kwamba hakuwa tayari kuwalea wanawe 3 katika ndoa yenye wake wengi kwa mume mmoja.

Kwa hiyo, Nderitu alifunga safari na wanawe wakaishia zao Marekani na kuapa kutompa Samidoh fursa ya kutangamana na wanawe, jambo ambalo hata hivyo lilikuja kuonekana kukiukwa hivi majuzi ambapo Samidoh alitembelea familia yake Marekani na kutangamana nao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved