Mkurugenzi wa blogu ya Kenya Online Media, Director Trevor ametoa taarifa baada ya ukurasa wa Facebook wa blogu hiyo kubadilishwa jina kwa muda.
Kupitia Instagram yake, Trevor alitaarifu mashabiki wake kwamba kulitokea hitilafu ambayo iliona ukurasa huo ukihaririwa jina na kuitwa ‘Mungai Eve Media’ – jina ambalo ulikuwa unaitwa awali kabla ya Trevor kubadilisha na kuita ‘Kenya Online Media’.
Alisema kwamba hitilafu hiyo ilitokea kwa ghafla na ilikuwa inashughulikiwa.
Hata hivyo, dakika kadhaa baadae, ukurasa huo uliweza tena kuhariri jina kutoka ‘Mungai Eve Media’ na kurejea kwa jina halisi la ‘Kenya Online Media’.
“Taarifa Kuhusu hitilafu ya Jina la Ukurasa wa Facebook. Wapenzi Wafuasi, Kwa sasa tunakumbana na tatizo la kiufundi na ukurasa wetu wa Facebook, ambalo limesababisha jina la ukurasa wetu kurejea kwa jina lake la asili, "Mungai Eve Media." Tafadhali tunahakikisha kwamba timu yetu inafanya kazi kwa karibu na Facebook ili kutatua suala hili haraka iwezekanavyo. Tunathamini uvumilivu wako na uelewa wako wakati huu. Asante kwa kuendelea kutuunga mkono,’ alitoa taarifa.
Ikumbukwe ukurasa huo ulikuwa unaitwa ‘Mungai Eve Media’ awali kabla ya Trevor kuamua kumfuta kazi Mungai Eve baada ya penzi lao kuyumba na kuanza kuuita ‘Kenya Online Media’.