logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkuu wa polisi amshauri Shakib kumfungulia Zari kesi ya ‘ukatili wa kiuchumi na kisaikolojia’

Polisi huyo alisema kuwa kesi kama hiyo inaweza kusajiliwa kwa polisi nchini Uganda.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 August 2024 - 06:58

Muhtasari


  • • Mvutano kati ya Shakib na Zari uliongezeka baada ya Zari kumkaribisha aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz, nyumbani kwake nchini Afrika Kusini kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yao.
ZARI NA SHAKIB

Mfanyibiashara Shakib Lutaaya Cham ameshauriwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mke wake, Zari Hassan, kufuatia mzozo unaoendelea katika uhusiano wao.

Jackson Mucunguzi, afisa mkuu wa polisi nchini Uganda, hivi majuzi alienda kwa X kumshauri kijana huyo kumfungulia Zari kesi kwa kile alisema kwamba mjasiriamali huyo mama wa watoto watano anamtumia vibaya kijana wa watu.

Mucunguzi alimshauri Shakib kwamba ikiwa anajua haki zake, anaweza kupiga hatua na kumfungilia Zari kesi ya ukatili wa nyumbani wa kiuchumi na kisaikolojia, baada ya mwanamama huyo kudai kwamba Shakib hakuwa anachangia chochote kiuchumi katika ndoa yao.

“Iwapo ndugu yangu Shakib akiwa mtu mzima atakusanya imani na kujua haki zake👮, kesi ya unyanyasaji wa kiuchumi na kisaikolojia wa nyumbani; inaweza kusajiliwa katika @PolisiUg, Idara ya Ulinzi wa Mtoto na Familia na kusikilizwa kwa mafanikio katika mfumo wa Haki wa Uganda,” Afisa huyo wa polisi aliandika, akisisitiza ni wakati maisha ya mtoto wa kiume pia yasingatiwe kuwa na umuhimu.

Mvutano kati ya Shakib na Zari uliongezeka baada ya Zari kumkaribisha aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz, nyumbani kwake nchini Afrika Kusini kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yao Latifah Dangote.

 

Katika ujumbe wake wa sauti, Lutaya, ambaye pia anajulikana kama Cham, alieleza kuwa vitendo hivyo vimemletea aibu mara kwa mara na kuathiri vibaya afya yake ya akili.

Akijibu, Zari ambaye alionekana kulewa na baadhi ya watazamaji alidai kuwa hakumualika Platnumz Afrika Kusini.

Pia alimkumbusha Shakib kwamba mwimbaji huyo wa Tanzania si tishio tena, akisema walikuwa wameshashibana miaka mingi iliyopita.

 

Zaidi ya hayo, alimwambia mume wake waziwazi kwamba hawezi kuweka sheria katika uhusiano wao kwani michango yake ni ndogo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved