logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Simple Boy na Dem wa FB wakichumbiana wana uwezo wa kuwa ‘power couple’ – Director Trevor

“Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza chumbiana wanaweza kuwa wachumba wa nguvu sana,”

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 August 2024 - 13:47

Muhtasari


  • • Alisema kwamba Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza kuchumbiana tu na kuwa wapenzi, penzi lao litakuwa la kupigiwa mfano na wengi.
DEM WA FB NA STEVO SIMPLE BOY.

Director Trevor amewashauri msanii Stevo Simple Boy na mchekeshaji Dem wa Facebook kufikiria suala la kuingia katika mahusiano.

Kwa mujibu wa Trevor, wawili hao wanaweza ungana pamoja na kufaidi pakubwa kutokana na umaarufu wao kaitka mitandao ya kijamii.

Alisema kwamba Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza kuchumbiana tu na kuwa wapenzi, penzi lao litakuwa la kupigiwa mfano na wengi.

“Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza chumbiana wanaweza kuwa wachumba wa nguvu sana,” Director Trevor aliandika katika picha ya pamoja na wawili hao.

Stevo na Dem wa FB ni wasanii wawili ambao wamezungumziwa mara nyingi kaitka mitandao ya kijamii kwa njia hasi, kutokana na mionekano yao wakiitwa ‘vienyeji’.

Msanii huyo wa Freshi Barida amekuwa akisuasua katika suala la maisha ya mapenzi, miaka miwili tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, Pritty Vishy.

Kwa upande wake, Dem wa Facebook ambaye amepata umaarufu hivi majuzi hayawahi weka wazi maisha yake ya kimapenzi, kwa wakati mmoja akisema kwamba hayuko tayari kujihusisha kimapenzi na mtu yeyote hadi pale atakapotimiza ndoto za kuwaweka wazazi wake katika maisha mazuri.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved